loader
Dstv Habarileo  Mobile
Tanapa yazindua mafunzo ya walimu

Tanapa yazindua mafunzo ya walimu

Kamishna Mwandamizi wa Uhifadhi Kanda ya Magharibi kutoka Shirika la Hifadhi ya Taifa (TANAPA) Martine Roiboki amezindua mafunzo ya siku tatu kwa walimu wa shule 23 zilizozunguka Hifadhi za Ibanda Kyerwa na Rumanyika Karagwe.

Mafunzo hayo yanayolenga kuwajengea uwezo walimu hao ili  kuwafundisha wanafunzi wa darasa la tano na kidato cha pili namna ya kulinda mazingira, kuhifadhi na kujitenga na maswala ya ujangili wanapohitimu shule za msingi na sekondari.

Mafunzo hayo yalihudhuriwa na walimu wa masomo ya Maarifa ya Jamii kwa Darasa la Tano, na masomo ya Geographia kidato cha pili ikiwa masomo yote hayo yanaelezea kwa undani maswala ya uhifadhi na utunzaji na athari zinazoweza kujitokeza kutokana na uchafuzi wa mazingira.

Mafunzo hayo yaliwashirikisha moja kwa moja walimu wa taaluma kutoka katika shule za msingi 19 zilizozunguka Hifadhi za Ibanda Kyerwa na Rumanyika Karagwe,na walimu wa sekondari nne zilizozunguka hifadhi hizo ,waratibu wa elimu kata zinakopatikana shule hizo,walimu wakuu wa shule hizo na maafisa Elimu wa Wilaya ili kusaidia kufundisha na kuwasimamia walimu wa Masomo hayo  kufundisha watoto kwa weledi na watoto hao baadaye kuwa mabalozi wazuri kwa Jamii juu ya kuepukana na ujangili katika Hifadhi za Taifa.

Kwa kujibu wa Kamishina huyo hifadhi tisa nchini ziko katika mpango wa kupata mafunzo kwa wanafunzi wa shule zilizozunguka hifadhi hizo ambapo wadau zaidi ya 500 watanufaika na mafunzo hayo na baada ya mafunzo  watawasimamia na kuwafundisha watoto namna ya kuhifadhi mazingira, madhara ya kutohifadhi mazingira ,namna ya kuelimiaha jamii kuepukana na  ujangili.

"Shirika la hifadhi nchini TANAPA kwa kushirikiana na Chuo kikuu Cha Dare es salaam kupitia serikali wizara ya  Elimu tuliona tuandae mpango wa   kuandaa watoto katika umri mdogo katika kujifunza kwa kina maswala yanayohusu Utalii na uhifadhi ,tukaja  na mpango wa awamu ya kwanza kwa  hifadhi 9 nchini  Baada ya mpango kwenda vizuri tunaweza kuzifikia shule zote nchini au serikali inaweza kuweka katika mitaala ya Elimu ili watoto wasome kwa urahisi ,matarajio yetu ni kuwa walimu waliofundishwa watakuwa Chachu kubwa ya kusimamia watoto wetu na kuwafundisha kikamilifu"alisema Loiboki.

Akizitaja hifadhi zilizopata mradi kuwa ni Hifadhi 9 ambazo ni Ibanda Kyerwa,Rumanyika Karagwe,Gombe,Kitulo,Mahale,Mikumi Udizungwa,Katavi na Saadani ambapo shule zilizozunguka hifadhi hizo zitanufaika moja kwa Moja na wadau Kama walimu ,wakuu wa shule,waratibu Elimu kata ,maafisa Elimu kata na Wilaya wapatao 500 watanufaika na Mafunzo kupitia mpango huo.

Aidha shule zitakazonufaika na mradi wa kuwafundisha wanafunzi juu ya uhifadhi watapata Fursa ya kuunda club za Mazingira shuleni na club hizo zitampa nafasi na Fursa  mwanafunzi yeyote wa darasa lolote kujiunga ambapo hata madarasa ambayo hayafundishi maswala ya uhifadhi na Utalii watajifunza kupitia club hizo zitakazoundwa shuleni.

Kamishina msaidizi wa uhifadhi Katika Hifadhi za Ibanda Kyerwa na Rumanyika Karagwe ,Moronda B Moronda alisema tayari wamepita katika shule zote za Kyerwa na kubaini kuwa Wilaya hiyo inawafaunzi laki moja (100,000)hivyo anaamini kuwa licha shule zilizopita katika mpango ni 23 lakini kupitia shule hizo huenda wanafunzi wote wakanufaika na Mafunzo juu ya uhifadhi na utunzaji wa Mazingira.

"Nashukuru shirika letu la hifadhi kuwa Hifadhi zote mbili ziko katika wilaya moja ya Kyerwa hivyo shule kupitia kwa walimu  waliopata bahati ya  kupata Mafunzo watakuwa wa kwanza kuleta matokeo chanya kwa shule nyingine ambazo hazipo katika mpango "alisema Moronda.

Hapo hawali mkuu wa wilaya ya Kyera Rashidi Mwaimu aliongea na wakuu wa shule na waratibu wa Elimu kata na Maafisa Elimu kuwa zoezi Hilo linapaswa  kuleta matokeo Chanya huku akiwataka wakuu wa shule kusimamia walimu kikamilifu juu ya ufundishaji wa Masomo yatakayomjenga mtoto Kupambana na maswala mbalimbali yanayoenda Kinyume na Utalii na uhifadhi.

Aidha alipongeza uwepo wa Hifadhi za Ibanda Kyerwa na Rumanyika Karagwe  kuwa kwa Sasa wananchi wanashuhudia uwepo wa mabadiliko makubwa Kama hewa nzuri katika maeneo yao,mvua za kutosha, kutokauka vyanzo vya maji, Wageni mbalimbali kutembelea hifadhi hizo   na hii inaonyesha ni kwa jinsi gani wananchi wakihifadhi Mazingira wanaweza  kupata matokea Chanya na kufurahia uhifadhi ,Tofauti na hasara lukuki zinazojitokeza pale wananchi wanapofanya ujangili,kufuga kiholela,na kufanya ujangili.

"Ofisi yetu kupitia idara ya Elimu iko tayari kuhakikisha mpango huu unatekelezwa kwa asilimia  100  na kupitia mpango huo jamii itaungana na watoto wao kupinga ujangili na kufanya uhifadhi endelevu  ambao utaendelea kupaisha Utalii kwa vizazi vijavyo"alisema Mwaimu

https://www.apps.tsn.go.tz/public/uploads/57b0a90789ee465f54f86954e815c38a.jpg

MAMLAKA ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya ...

foto
Mwandishi: DIANA DEUS

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi