loader
Dstv Habarileo  Mobile
Ajira 12,000 zanukia Tamisemi

Ajira 12,000 zanukia Tamisemi

OFISI ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) imeomba vibali vya ajira 12,000 kwa watumishi wa kada mbalimbali katika mwaka ujao wa fedha 2021/2022.

Hayo yalibainishwa na Naibu Waziri wa Tamisemi, Dk Festo Ndugange wakati akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Babati Vijijini Daniel Sillo (CCM) aliyetaka kujua mpango wa serikali katika kutatua tatizo la upungufu wa watumishi hasa katika elimu na afya katika jimbo lake.

Akijibu swali hilo, Dk Ndugange alisema ajira hizo zitakapotoka, maeneo yote yenye upungufu wa watumishi ikiwemo Babati Vijijini yatapewa kipaumbele.

Alisema moja ya sababu inayochangia kuwepo kwa upungufu wa watumishi katika halmashauri za vijijini ni kuhama kwa watumishi kwenda mijini mara tu wanapoajiriwa.

Katika swali lake la msingi, Mbunge wa Korogwe Vijijini Timotheo Mnzava (CCM), alitaka kujua ni namna gani serikali itatatua changamoto ya upungufu wa watumishi katika Halmashauri ya Wilaya ya Korogwe hasa kwenye Idara za Afya, Elimu na Kilimo.
Dk Ndugange alijibu kwa kusema kuwa kwa mujibu wa Ikama ya mwaka 2020/21, Halmashauri ya Wilaya ya Korogwe inapaswa kuwa na watumishi 2,630, lakini hadi mwezi Machi mwaka huu, Halmashauri ya Wilaya ya Korogwe ilikuwa na watumishi 2,294, hivyo ina upungufu wa watumishi 336 sawa na asilimia 12.8.

Pia alisema kwa mujibu wa Ikama Idara ya Afya katika Halmashauri ya Wlaya ya  Korogwe inapaswa kuwa na watumishi 392 lakini mwezi Machi mwaka huu, Idara ya Afya katika Halmashauri hiyo ilikuwa na watumishi 263, hivyo  ina upungufu wa watumishi 129 sawa na asilimia 32.9.

Kwa upande wa Idara za Elimu Msingi na Sekondari, alisema zinapaswa kuwa na watumishi 1,891 lakini zina watumishi 1,604, hivyo zina upungufu wa watumishi 287 sawa na asilimia 15.2 wakati Idara ya Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika inapaswa kuwa na watumishi 55 lakini ina watumishi 45, hivyo ina upungufu wa watumishi 10 sawa na asilimia18.2.

“Tamisemi imeendelea kuajiri na kuwapnaga watumishi wa kada mbalimbali katika halmashauri nchini ambapo katika mwaka wa fedha 2020/21 watumishi 81 wapya waliajirwa na kupangwa katika Halamshauri ya Wilaya ya Korogwe. Kati ya watumishi hao, 22 ni walimu wa shule za sekondari, 35 walimu wa shule za msingi, sita watumishi wa kada za afya na ofisa ugani mmoja,” alisema Dk Ndugange.

Alisema pamoja na jitihada hizo, katika Ikama na Bajeti ya mwaka 2021/22, Halmashauri ya Wilaya ya Korogwe imetenga nafasi za ajira mpya 150 kwa kada mbalimbali.

https://www.apps.tsn.go.tz/public/uploads/35851c5656766ed067da7f337ce661a6.png

MAMLAKA ya Kudhibiti na Kupambana na ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu, Dodoma

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi