loader
Dstv Habarileo  Mobile
Serikali yatekeleza miradi 355 ya maji na kunufaisha wananchi milioni 1.9

Serikali yatekeleza miradi 355 ya maji na kunufaisha wananchi milioni 1.9

SERIKALI kupitia Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) imetekeleza miradi 355 yenye thamani ya zaidi ya Sh bilioni 155.

Haya yameelezwa na Waziri wa Maji, Jumaa Aweso leo wakati wa kuwasilisha bungeni makadirio ya mapato na matumizi kwa mwaka 2021/22 kwa Wizara hiyo. Alisema kwa mwaka wa Fedha 2020/20210 RUWASA ilipanga kutekeleza jumla ya miradi 1,169.

Amesema,"Utekelezaji huo ulihusisha kukamilisha miradi iliyokuwa inaendelea, ujenzi wa miradi mipya, upanuzi na ukarabati wa miundombinu ya maji. Pia Serikali ilipanga kukarabati na kujenga mabwawa 19 na kufanya usanifu wa miradi 390. 

Aweso amesema hadi kufikia mwezi Machi 2021, utekelezaji wa jumla ya miradi 355 yenye jumla ya vituo vya kuchotea maji 6,687 umekamilika na kuanza kutoa huduma ya majisafi na salama kwa wananchi 1,984,575. 

"Utekelezaji wa miradi hiyo umegharimu kiasi cha shilingi bilioni 154.6. Aidha, utekelezaji wa miradi 814 iliyobaki unaendelea na upo katika hatua mbalimbali. 

Alisema Wizara kupitia RUWASA imefanya usanifu wa miradi 196 kati ya miradi 390 na kuchimba visima 155 katika vijiji 148, kufanya usanifu wa mabwawa matatu(Msanga na Pofu – Ikulu ya Chamwino na Sengenya ya Nanyumbu) na kuendelea na ujenzi wa mabwawa manne ya Nsekwa (Mlele).

Pia Ikozi (Sumbawanga), Chole (Kisarawe), Mwakijembe (Mkinga);na kukamilisha ukarabati wa bwawa la Vikonje lililopo Ikulu ya Chamwino. 

https://www.apps.tsn.go.tz/public/uploads/db84374cbd46433d2de64babe84ba3cc.jpg

MAMLAKA ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu,  Dodoma

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi