loader
Dstv Habarileo  Mobile
Ndege kutoka India zazuiwa kutua Dar

Ndege kutoka India zazuiwa kutua Dar

SERIKALI imezuia ndege zote zinazofanya safari za kwenda na kutoka nchini India kutokana na hali ilivyo kwa sasa ya maambuzi ya aina mpya ya virusi vya Covid-19.

Imesema kuwa zuio hilo lililoanza juzi litatekelezwa mpaka hapo itakapotolewa taarifa nyingine.

Hayo yameelezwa katika mwongozo mpya namba saba uliotolewa juzi na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto na kueleza kuhuishwa kwa mwongozo namba sita uliotolewa siku moja kabla ya huu wa sasa.

Katika taarifa hiyo iliyosainiwa na Katibu Mkuu Afya, Profesa Abel Makubi, ilieleza kuwa hatua hiyo inatokana na kasi ya mlipuko wa ugonjwa huo hivyo serikali imezuia ndege zote zinazoingia na kutoka nchini kutokea India.

Profesa Makubi alieleza kuwa zuio hilo halitahusu zile za mizigo ambazo zitaendelea kuingia nchini. Hata hivyo, alisema   wafanyakazi wa ndege hizo hawataruhusiwa kushuka na ndege nyingine kutoka India zitakazoruhusiwa ni zile zilizoidhinishwa na mamlaka kufanya shughuli za kibinadamu, diplomasia na kutoa misaada ya matibabu.

Mwongozo huo ulibainisha kuwa Watanzania wanaorejea nchini kutoka India kama vile wanafunzi, wafanyabiashara au wanaotoka kupata matibabu wanatakiwa kufuata taratibu zilizowekwa ikiwemo kupima virusi hivyo na kisha kukaa karantini siku 14 kwa gharama zao.

Ilieleza kuwa abiria watakaoingia nchini watatakiwa kukaa karantini kwa lazima na gharama zao kwa kuchagua maeneo ya kukaa yaliyopo katika viwanja vya ndege au katika mtandao wa Wizara ya Afya yaliyotengwa na serikali huku Watanzania wanaoingia nchini kutoka India wataruhusiwa kujitenga wenyewe katika nyumba zao.

“Ikiwa abiria atawasili katika uwanja wa ndege, bandari au kituo chochote kutoka nje ya nchi, watapatiwa kadi ya taarifa za afya na kupatiwa namba kisha kushauriwa kujiangalia wenyewe iwapo wataona dalili za ugonjwa, na iwapo watabaini dalili zozote watapimwa na kupatiwa matibabu na serikali kwa gharama zao,” alieleza Profesa Makubi.

India ilianza kukabiliwa na aina mpya ya ugonjwa wa Covid-19 Machi mwaka huuu na kusababisha idadi kubwa ya vifo na mashirika ya misaada kupeleka vifaa vya matibabu vya dharura kusaidia kuzuia ongezeko la wagonjwa.

Ofisa wa Kituo cha Kitaifa cha Kudhibiti Magonjwa alisema kuibuka kwa ugonjwa huo kunatokana mlipuko wa awamu ya pili na mpaka juzi, India iliripoti maambukizi ya watu 412,000 kwa saa 24 na vifo 3,980. 

Katibu Mkuu Afya alibainisha kuwa abiria waliosafiri kwa zaidi ya saa 72 watatakiwa kupimwa tena wanapowasili nchini huku wafanyakazi wa kwenye ndege wakitakiwa kuchukua tahadhari zinazostahili na kuonesha vyeti vinavyoonesha kupimwa ugonjwa huo.

Aliongeza kuwa abiria wote watakapowasili nchini, watawasilisha cheti kinachoonesha wamepima na kuwa hawana maambukizi ya virusi hivyo na kuwa wamepimwa ndani ya saa 72 kabla ya kuwasili nchini.

Alisema mikakati ya nyongeza kwa madereva wa magari na malori yanayobeba bidhaa na kutoa huduma mbali mbali kuwa wanatakiwa kuwa watu wawili hadi watatu katika kila gari na katika safari zao wanaruhusiwa kusimama katika vituo vilivyoainishwa na serikali.

Alisema ikiwa mmoja wa watu katika magari hayo atawekwa karantini akiwa safarini, mmiliki wa magari hayo atahakikisha hatua kumhudumia mfanyakazi wake na pia gari hilo na kuhakikisha bidhaa zinafika katika maeneo yaliyotarajiwa.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/080916223a07810eaf08959aff6d944d.jpeg

MAMLAKA ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya ...

foto
Mwandishi: Theopista Nsanzugwanko

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi