loader
Dstv Habarileo  Mobile
Samia kuteta na wazee 900 leo Dar

Samia kuteta na wazee 900 leo Dar

RAIS Samia Suluhu Hassan leo anatarajiwa kufanya mkutano na wawakilishi wa wazee 900 wa Mkoa wa Dar es Salaam na watatumia fursa hiyo kujadili mambo mbalimbali.

Mkuu wa Mkoa wa Dar se Salaam, Abubakar Kunenge alisema jana kwamba kikao hicho kitafanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Mlimani City, Barabara ya Sam Nujoma kuanzia saa 8:00 mchana.

Kunenge alitoa wito kwa waze waliopata mwaliko wa kushiriki katika kikao hicho kujitokeza kwa wingi ili kupata kusikiliza kile ambacho Rais Samia alichowaitia.

“Ni muhimu kujali muda ili kuondoa usumbufu kwa wazee wetu na kuhakikisha wanapata mahali sahihi pa kuketi wakiwa tayari kusubiri kuzungumza na Rais wao,” alisema Kunenge.

Aidha, mkuu wa mkoa alisema wa wale wazee pamoja na Watanzania wengine ambao hawakupata mwaliko wa kukutana na Rais Samia katika kikao hicho, basi wanaweza kufuatilia mkutano huo kupitia vyombo vya habari.

Kwa upande wa baadhi ya viongozi wa wazee walioalikwa, walimshukuru Rais Samia kwa kuona umuhimu wa kukutana na wazee huku wakisema wanatarajia kikao hicho kitakuwa na manufaa makubwa kwao.

Hii itakuwa ni mara ya kwanza kwa Rais Samia kuzungumza na wazee wa Mkoa wa Dar es Salaam, wazee wengine nchini na Watanzania kupitia vyombo vya habari tangu ashike madaraka hayo Machi 19, mwaka huu.

Atazungumza na wazee hao siku mbili tangu arejee nchini baada ya ziara ya kikazi ya siku mbili nchini Kenya kwa mwaliko wa Rais Uhuru Kenyatta.

Marais wa Tanzania wamekuwa na desturi ya kukutana na wazee hasa wa Dar es Salaam wakiwakilisha wenzao wengine, wanapokuwa na jambo wanalotaka ama kuongea nao au kuzungumza na taifa kwa ujumla.

Watangulizi wa Rais Samia, Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere, Mzee Ali Hassan Mwinyi, Benjamin Mkapa, Jakaya Kikwete na Dk John Magufuli, wamefanya hivyo mara kadhaa wakati wa uongozi wao.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/c95bd0e1ca47bf8172ab9a800ed080c1.jpeg

MAMLAKA ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi