loader
Dstv Habarileo  Mobile
Shirika lawajengea uwezo waandishi wa habari wanawake

Shirika lawajengea uwezo waandishi wa habari wanawake

SHIRIKA la Friedrich Naumann Foundation For Freedom, limewajengea uwezo waandishi wa habari wanawake 16 kutoka nchini Kenya na Tanzania ili wapige hatua zaidi kwani wengi wao hawachangamkii fursa zilizopo.

Ofisa Mipango wa Shirika la Friedrich Naumann Foundation For Freedom, Veni Swai alisema hayo wakati wa kuhitimisha mafunzo ya kuwajengea uwezo waandishi hao wanawake yaliyofanyika jijini Nairobi nchini Kenya.

Alisema katika mafunzo mengine waliyowahi kuyatoa kwa wana habari wamegundua wanawake wachache ndio walioshiriki wengi wao walikuwa na visingizio vya kuwafanya wasishiriki.

“Kwenye mafunzo yale ya mwaka jana wanawake wengi walikuwa na visingizio kwani kati ya waandishi 17 tuliofanya nao kazi wanawake walikuwa ni watano, na kati ya hao watano wawili wakaishia njiani wakabaki watatu,” alisema.

Alisema imekuwa ni kawaida kwa waandishi wa habari wa kike kutokujipa kipaumbele kwenye nafasi mbalimbali hivyo shirika hilo limeona lisiache jambo hilo liendelee bali lijenge uwezo zaidi kwao.

“Tulitafuta namna ya kuwapa nafasi wanawake pengine wangesema nini kinawasibu katika kazi yao ya uandishi wa habari,” alisema.

Kwa upande mwingine Veni alisema shirika hilo limekuwa likifanya kazi za haki za binadamu ambazo wanakutana na kadhia zinazowakumba waandishi hao wa kike.

Alisisitiza kuwa kwa kutoa kipaumbele kwa wanawake kutasaidia kutambua nafasi na fursa walizonazo kwani shirika hilo linafanya kazi mbalimbali za kuwajengea uwezo wadau mbalimbali wakiwemo pia viongozi, vijana pamoja na wanawake.

Kwa upande wake Mkufunzi wa mafunzo hayo kwa waandishi wa habari 16 kutoka nchini Kenya na Tanzania, Njeri Kabeberi alihimiza juu ya kujitambua, kupanga ratiba ya kazi, kufanya kazi zenye ubora kwa malengo ikiwa ni pamoja na kuachana na mambo yanayoweza kupoteza muda bila sababu ya msingi.

Pia alihimiza juu ya kutafuta fursa ikiwa ni pamoja na kuwa na malengo ya kusonga mbele yaani kutoka hatua moja kwenda nyingine.

Kwa upande wa waandishi wa habari waliohudhuria mafunzo hayo ya wiki nzima walieleza jinsi wanavyokutana na misukosuko katika kazi lakini wanapambana ili kusonga mbele.

https://www.apps.tsn.go.tz/public/uploads/635b437bf9f7a22bc45365879c7b95bc.jpg

MAMLAKA ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya ...

foto
Mwandishi: Lucy Ngowi

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi