loader
Dstv Habarileo  Mobile
BASATA YAFUNGUKA KUUFUNGIA WIMBO WA NEY WA MITEGO

BASATA YAFUNGUKA KUUFUNGIA WIMBO WA NEY WA MITEGO

Kaimu Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa Taifa ( BASATA ) Matiko Aniko ameeleza kuwa baraza hilo lilimpa maelekezo msanii wa muziki wa ‘Hip Hop’ Emmanuel Elibariki ‘Ney wa Mitego’ kurekebisha mashairi ya wimbo wake wa Mama lakini hakufanya hivyo.

Siku nne zilizopita BASATA iliufungia wimbo huo kutokana na utata wa mashairi yake kwa kushindwa kufuata maadili na kanuni za baraza hilo.

Akizungumza mapema leo kwenye kipindi cha XXL, kinachorushwa na CLOUDS FM, Kayanga amesema ni utaratibu wa baraza kukagua wimbo wa msanii yoyote kabla ya kuachia kwa lengo la kujiridhisha kama unafaa kulingana na kanuni.

"Utaratibu wa kukagua ni wa siku zote, hadi leo tumeshakagua kazi zaidi ya elfu 12 na kati ya hizo ni kazi 14 tu ndizo ambazo zimekataliwa na kutakwa zikafanyiwa marekebisho" amesema Matiko.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/2ddf15d06b613dcad808e920eaef2af9.jpeg

YANGA leo saa 1:00 usiku itashuka dimbani kuikabili ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi