loader
Dstv Habarileo  Mobile
Namungo  hasira zote kwa KMC

Namungo  hasira zote kwa KMC

BAADA ya kupoteza mchezo wa kiporo kwa bao 1-0 dhidi ya JKT Tanzania, kocha mkuu wa timu ya Namungo, Hemed Suleiman ‘Morocco’ , amesema kuwa anautumia mchezo wa KMC kurudisha imani katika kikosi chake.

Mchezo huo wa kiporo uliochezwa katika Uwanja wa Jamuhuri, umewafanya wasalie katika nafasi ya 12 wakiwa na pointi zao 32 katika msimamo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara.

Akizungumza na gazeti hili jana Morocco  alisema kuwa  baada ya kupoteza mchezo wa ugenini dhidi ya JKT Tanzania sasa hasira  zao watamalizia kesho kwa KMC watakapokuwa nyumbani katika Uwanja wa Majaliwa.

“Tumefungwa bao 1-0 na JKT pale jijini Dodoma jambo ambalo ni kinyume na malengo yetu, sisi hatutaki kupoteza mechi, kwa hiyo lazima mchezo wetu unaofuata tushinde ili tujipoze machungu,”alisema.

Alisema kuwa wanaiheshimu KMC ni timu nzuri na ina wachezaji wazuri, lakini hata Namungo wapo vizuri na kwa kudhihirisha hilo wanataka kushinda kesho na kujiweka katika mazingira mazuri zaidi katika msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/25871244ef8d97307da38dbd203e0b53.jpeg

YANGA leo saa 1:00 usiku itashuka dimbani kuikabili ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi