loader
Dstv Habarileo  Mobile
Tunapofungia muziki tunajua maana yake?

Tunapofungia muziki tunajua maana yake?

KWA watu wanaojua muziki, kwanini upo na kwanini hubadilika wanaweza kabisa kukubaliana nami kwamba Baraza la Sanaa la Taifa (Basata) na viongozi wengine wanalipuka katika maamuzi yao, kupotosha maana ya muziki (sanaa) na  mbaya zaidi kukwamisha wanaotegemea muziki kuishi.

Pamoja na hayo kupunyua mistari ni tendo ovu dhidi ya sanaa ya muziki kwa dai la kuendeleza utamaduni wa taifa dhana ambayo mimi naiona kuwa dhaifu.

Nasema hivyo kwa kuamini kwamba katika nchi yenye makabila zaidi ya 120 kuwa na  mtiririko mmoja wa muziki  katika majira tofauti ya muziki, kunaamananisha kwamba  kazi kubwa ya Basata ni kutaka tuwe na nyimbo za taifa na hapa inaudhi kwani aina ya nyimbo ni nyingi  hivyo si sahihi kuamua kufungia muziki ila inafaa kuuelekeza katika majira yake.

Kutokana na ukweli unaohusu muziki ( nyimbo) kuingilia mashairi yake ni kujitia kitanzi cha kazi ya sanaa ambayo inatakiwa kuwa huru. Tuko katika dunia ambayo fikra hufanyiwa kazi kwa namna inayofaa kwani huwezi kusikia nyimbo za kufunda mwali hadharani lakini faragha wenyewe huziimba.

Muziki  kwa mimi niliyesoma zama hizo ni aina ya fasihi simulizi inayowasilishwa kwa hadhira kwa njia ya uimbaji au ughani badala ya usemaji wa kawaida. Katika hili kuna vitu viwili ambavyo ni nyimbo na maghani.

Inatupasa tuelewe kwamba nyimbo ni kila kinachoimbwa ambapo ndani kuna kipera kimegawanyika katika vijipera vifuatavyo ambavyo ni, tumbuizo, bembea, kongozi, nyimbo za dini, wawe, tenzi, tendi, mbolezi, kimai, nyiso, nyimbo za vita, nyimbo za uwindaji, nyimbo za taifa, nyimbo za watoto na nyimbo za kazi.

Kutokana na uwapo wa vipera ni dhahiri kitendo cha kumwambia mtunzi abadilishe maandiko yake ni usumbufu ambao sio sawasawa lakini la maana ni kutambua huo wimbo ulikuwa wa kongozi yaani kuaga mwaka, wawe yaani  za kulimia au tendi yaani masimulizi ya matendo ya mashujaa.

Naamini kabisa kwamba katika upana wake wa  fasihi  hatutakuwa tunaifanyia neema tasnia ya muziki  kwa kulazimisha watu wote watunge  nyimbo za taifa yaani nyimbo za kusifia taifa au kabila au nyimbo za kazi.

Kitendo cha Basata kupitia mistari, kuirekebisha ni kitendo cha hovyo kabisa ambacho mimi naamini kinaleta shida katika tunzi na maana ya utunzi kwani tangu zamani zaidi ya miaka 50,000 iliyopita katika Afrika, watu hutoa hisia zao kwa njia ya muziki. Ni ubunifu huo ndani ya muziki unapata ladha inayotakiwa kwa majira takiwa.

Kuuchambua muziki kwa sababu za kuukataza ni kuharibu sanaa na ufundi anaoutumia mwanadamu ili kuwasilisha fikra au mawazo yaliyo ndani ya akili yake kwa hadhira.

Na ili tusiharibu hiyo sanaa (kwani huibua uzuri wake uliosanifiwa) ili kuvutia watu kwa uzuri wake na mguso ni heri Basata ikaweka madaraja kwenye mambo yake mathalani kusema  muda wa muziki huo kutumika au chombo kinachostahili kutumika vinginevyo tutakuwa watu tusiojua thamani ya kazi ya sanaa na wavurugaji wa uhuru wa kujieleza.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/c9ec260ca85d30fcef2ec6bb07d05cbf.jpeg

LIGI Kuu ya Tanzania inaelekea ukingoni ...

foto
Mwandishi: Beda Msimbe

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi