loader
Dstv Habarileo  Mobile
Dk Mwinyi apokea mpango wa ujenzi wa bandari ya mafuta

Dk Mwinyi apokea mpango wa ujenzi wa bandari ya mafuta

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk Hussein Mwinyi, amesema Zanzibar iko tayari kutekeleza mpango wa ujenzi wa bandari ya mafuta katika eneo la Mangapwani. 

Dk Mwinyi alisema hayo Ikulu,  Jijini Zanzibar baada ya kupokea Mpango wa ujenzi wa Bandari ya Mafuta katika eneo la Mangapwani Mkoa wa Kaskazini Unguja, uliotayarishwa  na Mamlaka ya Uwekezaji ya Oman (OIA). 

Alisema serikali hivi sasa iko tayari kuanza majadiliano ya kina na wawekezaji wenye nia ya kuwekeza katika eneo hilo, baada ya kupokea mpango huo unaobainisha maeneo tofauti  na kuwa bandari tofauti zitajengwa.

Alisema wakati mchakato wa utayarishaji wa mpango huo ukiendelea kuna  wawekezaji kadhaa waliojitokeza na kuonyesha nia ya kuwekeza katika miradi tofauti, hivyo akatoa wito kwa wawekezaji wa ndani na  nje ya nchi kujitokeza na kuwekeza.

Aidha aliishukuru Mamlaka ya Uwekezaji ya Oman kwa kushirikiana kikamilifu na watendaji wa serikali na hatimaye kufanikisha kazi hiyo muhimu kwa wakati muafaka na kwa ufanisi mkubwa. 

Mapema, akiwasilisha mpango wa ujenzi huo, Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Uwekezaji ya Oman (OIA) Sheikh Mohamed Al Tooqi, alisema mpango huo mkubwa  unahusisha maeneo makuu matatu, ikiwemo ujenzi wa bandari mbali mbali, mji wa kisasa wa makazi pamoja na Mpango wa kuiendeleza Bandari ya Malindi ili iweze kutumika kama Bandari ya utalii.  

Viongozi mbalimbali wa Kitaifa walishiriki katika hafla hiyo ya kupokea Mpango wa  Ujenzi wa Bandari ya Mafuta Mangapwani, akiwemo Balozi Mdogo wa Oman  Sheikh Mohamed Ibrahim Al-Bulushi, Mawaziri, Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar Dk Mwinyi Talib Haji, Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Mhandisi Zena Ahmeid Said, Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi Idrissa Kitwana Mustafa, Wakuu wa Vikosi vya Ulinzi na Usalama pamoja na watendaji kutoka taasisi na Idara mbalimbali za serikali.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/ca8fc8bd078ca1179576c8a79c692850.jpg

MAMLAKA ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Maalum, Zanzibar 

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi