loader
Dstv Habarileo  Mobile
Heri ya Siku ya Mama, tuitumie kuthamini malezi yao

Heri ya Siku ya Mama, tuitumie kuthamini malezi yao

LEO ni siku ya mama duniani ambayo inaadhimishwa kila Jumapili ya pili ya mwezi Mei kwa nia ya kuonyesha heshima na thamani ya akina mama katika familia kutokana na mchango na ushawishi wao mkubwa katika jamii.

Siku hii inatumika kuwaenzi akina mama kutokana na mchango wao katika malezi , ustawi na maendeleo kwa jamii ,nchi na ulimwenguni huku kwa wale waliokosea akina mama kuomba msamaha na kuweka vizuri mahusiano nao .

Kuna usemi unaosema “nani kama mama” kwa kweli wote tutakubaliana kuwa hakuna anayeweza kuchukua nafasi ya mama kwa yale wanayotenda kwa watoto wao waliozaa na hata watoto waliowalea hivyo ni vema kutumia siku hii kutambua mchango wao katika maisha ya kila mmoja wetu.

Ni dhahiri kuwa wapo wanaofahamu changamoto kadhaa wanazokumbana nazo akina mama kwenye malezi na hata ujenzi wa familia lakini bado hawakati tamaa hata kama ana changamoto vipi bali atahakikisha watoto na familia nzima inakuwa na amani na maendeleo.

Miaka ya hivi karibuni kumekuwa na baadhi ya akinamama wamepoteza maisha kutokana na changamoto za familia na mahusiano na hata kusababisha kupoteza maisha kwa kile kinachoelezwa kutunza watoto na familia zao.

Katika kuadhimisha siku ya leo ni vema kuhakikisha kila mmoja anaonesha upendo kwa akina mama kwa kuwafanyia vitendo vya ukarimu na kuwapongeza kwa yote waliyotutendea kwani ni dhahiri kuwa haiwezekani kumlipa mama kwa yale aliyotenda.

Ni vema katika sikukuu hii ni vema kuhakikisha wale wanao kama unapata bahati ya kuwa na mama mzazi au mlezi akiwa hai kumpeleka zawadi ,kula chakula pamoja naye na hata kukaa na kuzungumza naye masuala kadhaa yanayohusu maisha.

Kwani kuna baadhi ya mambo ambayo akinamama wamekuwa wakinyamanza kimya hata wanapopata changamoto hivyo ni vema kutumia siku hii kuzungumza nao ili waweze kutoa yale yaliyo katika mioyo yao na hata kwa walio mbali kupata muda wa kuzungumza nao kwa simu kwa muda mrefu.

Iwapo kuna waliowakwaza akina mama ni vema kuomba msamaha kwa vitendo hivyo ili kupata msahama na kamwe wasikubali kuwa na changamoto, na mama hata pale anapokosea ni vema kutumia busara kumaliza tofauti kwani nao ni biandamu wanaweza kukosema.

Heri ya Sikukuu ya Akinamama wote kwani hakuna kama mama katika dunia hii, na ni nafasi kwa wanawake walioolewa kuwafanya mama wakwe kuwa ni akina mama kwa kuzaa na kuwalea wanaume waliowaoa.

Ni vema kumfanya mama mkwe kama mama mzazi na kupokea mapungufu aliyonayo na kamwe usikubali kuwa na makwazo na mama mkwe, kwani usipokuwa rafiki na mama wa mume wako hata mume wako hatafurahi hata kama hatakuonesha hivyo ni vema kutambua hakuna kama mama.

Katika siku hii ni vema kama una mama mkwe aliyemzaa mumeo au aliyemlea ni vema ukahakikisha unamuwezesha kufurahia na mwanaye kwa lengo la kuthamini mchango wake katika malezi ya mumeo na familia yao.

Kila la heri kwa akinamama wote kwa kusheherekea siku hii na pia kuomba Mungu awasamehe makosa yao na kuwapumzisha kwa amani akinamama wote waliotangulia mbele ya haki kwa mema waliyotenda wakati wa uhai wao.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/e6992e0c764c52b10326c682b38d8394.jpeg

KWA miongo kadhaa kumekuwa na mjadala ...

foto
Mwandishi: Theopista Nsanzugwanko

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi