loader
Dstv Habarileo  Mobile
Samia ataka dini zidumishe amani

Samia ataka dini zidumishe amani

RAIS Samia Suluhu Hassan ametoa mwito kwa viongozi wa dini kuendelea kuimarisha na kudumisha ushirikiano kati ya dini moja na nyingine kwa ustawi wa amani ya nchi.

Aidha, amewataka viongozi wa dini waendelee kuhubiri amani ikiwa ni pamoja na kukemea vitendo viovu miongoni mwa jamii hasa vijana.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa aliyasema hayo jana katika Kanisa Kuu Usharika wa Lushoto alipomuwakilisha Rais Samia katika hafla ya kuwekwa wakfu na kuingizwa kazini Askofu Mkuu wa Kanisa la KKKT Dayosisi ya Kaskazini Mashariki, Dk

Msafiri Mbilu.

Dk Mbilu anakuwa Askofu Mkuu wa tano wa Kanisa la KKKT akichukua nafasi ya Askofu Steven Munga.

Rais Samia alimtaka Askofu Dk Mbilu imani yake iwe ni chachu ya kutenda kazi ya Mungu.

“Nakupongeza sana kwa kupewa jukumu hili kubwa tuna imani utalitumikia kanisa kwa moyo na imani kwa waumini wanaokuzunguka kutoka serikali inatambua michango wa taasisi za dini kutoa huduma za jamii,” alisema Majaliwa.

Akaongeza: “Natoa mwito kumpa ushirikiano wa kutosha na tunahitaji kuwa na ushirikiano kwa dini zote na tuombee taifa kutokana na

majanga mbalimbali na hili limethibitishwa katika kipindi cha ugonjwa wa corona, kimbunga Jobo hayo yote ni maombi yenu.”

Kuhusu huduma za jamii, Waziri Mkuu Majaliwa alisema serikali inatambua michango ya taasisi za dini katika huduma za jamii kama elimu, afya, maji na kwamba, serikali itaendelea kutoa ushirikiano ili kila mwananchi apate huduma pale alipo.

“Serikali inatambua mchango wenu nayo inasaidia kutoa huduma na tutaendelea kutoa ushirikiano ili kila Mtanzania anufaike,” alisema.

Kuhusu suala la Chuo Kikuu cha Sekomu kufunguliwa, amewataka viongozi wa kanisa hilo kufuata taratibu

ili kiweze kuanza kazi huku changamoto nyingine zikiwemo madeni na wahadhiri wenye sifa zikendelea kutatuliwa na kuwataka kanisa hilo kujiimarisha kiuchumi kwa kutumia fursa za bomba la mafuta na kilimo kujiimarisha kiuchumi.

Mkuu wa KKKT Tanzania, Askofu Dk Federick Shoo alitoa maombi mawili ya kupunguziwa mzigo wa kodi katika vituo vya huduma za elimu kwa shule za sekondari, vyuo na vituo vya Afya na hospitali pia suala la vibali vya kuishi nchini kwa wamisionari wanofanya kazi za kujitolea.

Askofu Mbilu aliahidi kutatua changamoto zilizoikumba dayosisi hiyo katika kipindi cha mpito.

foto
Mwandishi: Cheji Bakari, Tanga

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi