loader
Dstv Habarileo  Mobile
Juventus kufukuzwa Serie A 

Juventus kufukuzwa Serie A 

RAIS wa Chama cha soka Italia FA Gabriele Gravina amesema Juventus huenda ikafukuzwa kwenye Serie A kama hawatajitoa kwenye European Super League.

Timu hiyo ilikuwa miongoni mwa wimu 12 zilizoungana kwa ajili ya kuanzisha European Super League kabla ya timu sita za England hazijajitoa.

Timu zilizojitoa ni Chelsea, Manchester City, Manchester United, Tottenham Hotspur, Liverpool na Arsenal. Timu hizo zilijitoa siku mbili baada ya ligi hiyo kutangazwa kutokana na mashabiki wao kutaka wajitoe. 

Inter Milan na Atletico Madrid zilifuatia kujitoa kabla AC Milan kukiri kwmaba haikuwa na chaguo lingine. Lakini Juve, Real Madrid na Barcelona hazijatangaza kujitoa kwenye ligi hiyo. 

Chanzo kilisema timu hizo zinakabiliwa na adhabu ya kufungiwa miaka miwili kushiriki michuano ya Uefa kama hazitatangaza kujitoa kwneye ligi hiyo. 

"Sheria ziko wazi,” Gravina aliiambia Radio Kiss Kiss Napoli. "Kama usajili wa msimu ujao utaanza na Juve bado iko sehemu ya Super League, hawataruhusiwa kushiriki Serie A.

"Itakuwa aibu kwa mashabiki wote, lakini kuna sheria na zinatumika kwa kila mmoja.”

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/3b648b93a0a3de0553eb7db9117da3f9.jpeg

Kocha Gennaro Gattuso anatarajia kuondoka katika ...

foto
Mwandishi: TURIN, Italia

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi