loader
Wanafunzi wanaopata ujauzito kuendelea na masomo

Wanafunzi wanaopata ujauzito kuendelea na masomo

WIZARA ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imesema inaweka utaratibu kuwawezesha wanafunzi watakaopata ujauzito waendelee na masomo kupitia elmu mbadala.

Watakaofanya vizuri kimasomo katika mfumo mbadala huo, watarudishwa kwenye mfumo wa kawaida wa elimu.

Hata hivyo kwa mujibu wa Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako, kurudi katika mfumo wa kawaida wa elimu kutategemea mwanafunzi huyo aliacha shule akiwa katika hatua gani.

Ndalichako alibainisha hayo alipokuwa katika Shule ya Sekondari Kibasila iliyopo Dar es Salaam wakati Waziri wa Uingereza anayeshughulikia masuala ya Afrika, James Duddridge alipotembelea shule hiyo.

Alitoa mfano kuwa, kama mwanafnzi aliacha masomo akiwa kidato cha kwanza, anaweza kusoma kupitia mfumo huo wa elimu mbadala na akifika kidato cha pili, atafanya mtihani na akifaulu atarudishwa kwenye mfumo wa kawaida.

"Vile vile yule ambaye aliacha akiwa kidato cha tatu, akifanya mtihani wake kupitia mfumo usio rasmi akafaulu mtihani wa kidato cha nne, anapata fursa sawa kama yule aliyekuwa shuleni kupangiwa katika shule yoyote kutokana na ufaulu wake,” alisema Profesa Ndalichako.

Akaongeza; "Tutaendelea kuhakikisha kuwa tunasimamia elimu kwa watoto wa kike na kuondoa vikwazo vinavyosababisha watoto wa kike wasifanye vizuri katika masomo yao sambamba na kuboresha elimu kwa jumla ili wote watoto wote wa kike na wa kiume wapate elimu bora."

Alisema Uingereza imetoa fedha kukarabati wa Shule ya Sekondari Kibasila ambayo awali ilikuwa na majengo chakavu.

Naibu Waziri kutoka Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), David Silinde, alisema fedha zinazotoka kwa wafadhili ikiwemo serikali ya Uingereza, zikifika zinapitia Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolpjia kisha Ofisi ya Rais Tamisemi.

"Hata wao watu wa Uingereza moja ya mambo waliyoangalia ni kuona namna gani ‘force account’ inatekelezeka. Sisi tunawashawishi kuwa tuna miradi mingine wakileta fedha tutafanya zaidi," alisema Silinde.

"Nimeona pia elimu ya mtoto wa kike inazingatiwa hapa nchini, hivyo tutaendelea kushirikiana na serikali katika kukuza na kuendeleza maendeleo ya mtoto wa kike ili aweze kusoma katika mazingira mazuri," alisema.

Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Kibasila, Patrick Sinyinza, alisema msaada wa ukarabati wa majengo na ujenzi wa majengo mengine umesaidia kuongeza idadi ya wanafunzi wa kidato cha kwanza kutoka 240 hadi 340 kwa mwaka wa masomo 2021.

Sinyinza alisema pia kidato cha tano kwa mwaka huu wa masomo wamechukua wanafunzi 350 badala ya 155 waliokuwa wakisajiliwa awali.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/31f08aaab9b069b8249ba3c08f7d1ca4.jpeg

WAFANYAKAZI wa Kituo cha Redio ...

foto
Mwandishi: Lucy Ngowi

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi