loader
Dstv Habarileo  Mobile
Mkenda amuonya Mtendaji Mkuu Tume ya Ushirika

Mkenda amuonya Mtendaji Mkuu Tume ya Ushirika

WAZIRI wa Kilimo, Profesa Adolf Mkenda, amemtaka Mrajisi na Mtendaji Mkuu wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika nchini, Dk Benson Ndiege, ajitathmini na aache mzaha.

Waziri Mkenda alisema hayo jana na akaagiza Kaimu Mrajis Msaidizi wa Vyama Vya Ushirika Mkoa wa Lindi, Edmund Masawe, asimamishwe kazi.

“Mrajisi ‘watch out’ (angalia sana) uwezo wa kukung’oa ninao,” alisema Profesa Mkenda wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma.

Alisema katika kikao kazi Mrajis na Mtendaji Mkuu wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika nchini aliagizwa atoe taarifa ya ushauri wake kuhusu mradi wa pamoja wa vyama 32 vya msingi vya ushirika (G32) vya mkoani Kilimanjaro, lakini hakufanya hivyo na badala yake alikwenda kuifuta G32.

“Katibu Mkuu mimi nadhani Mrajis wa Vyama vya Ushirika anafanya mzaha, anadhani siwezi kumng’oa na pengine mahali pa kuanza kupafumua katika Wizara ya Kilimo ni Tume ya Maendeleo ya Ushirika,” alisema Profesa Mkenda.

Alisema amemuweka Ndiege katika uangalizi maalumu na akamuagiza ifikapo Mei 17, mwaka huu, afike kwake na awasilishe mapendekezo hayo.

Kuhusu Mrajisi Msaidizi wa mkoani Lindi, alisema anasimamishwa kazi kwa kuwa alilazimisha Chama cha Ushirika wa Mazao (AMCOS) cha Umoja kilichopo Wilaya ya Liwale mkoani Lindi kukodi ghala kwa ajili ya kuhifadhi korosho wakati chama hicho kina ghala lake la kuhifadhia zao hilo.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/1bf474a842dc076cefaa678a0622badf.jpeg

MAMLAKA ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya ...

foto
Mwandishi: Sifa Lubasi, Dodoma

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi