loader
Yanga yaikabili Namungo Lindi leo

Yanga yaikabili Namungo Lindi leo

LIGI Kuu Tanzania Bara, inataraji kuendelea tena leo kwa timu sita kushuka kwenye viwanja vitatu tofauti kusaka pointi tatu ili kujiweka katika mazingira salama kwenye msimamo.

Namungo FC watakuwa nyumbani Uwanja wa Majaliwa kuwakabili Yanga, mchezo ambao unatarajiwa kuwa na ushindani na kufuatiliwa na mashabiki wengi wa soka.

Timu hizo mbili zinakutana zikiwa nafasi tofauti wenyeji Namungo wakiwa nafasi ya 10 kwenye msimamo, wamecheza michezo 25 na wana pointi 35, wakati Yanga inashika nafasi ya pili kwenye msimamo wakiwa na pointi 57 na baada ya kucheza michezo 27.

Katika mchezo wa mzunguko wa kwanza zilipokutana Uwanja wa Mkapa, timu hizo zilitoka sare ya kufungana bao 1-1.

Namungo hawapo kwenye mwenendo mzuri katika ligi hiyo licha ya kushinda mchezo uliopita dhidi ya Mtibwa Sugar, bado kiwango cha timu hiyo hakiridhishi jambo linalo wapa nafasi

wageni wao Yanga kufanya vizuri kutokana na ubora waliouonesha siku za karibuni wakiwa kocha Nasredden Nabi.

Kocha Hemed Seleman ‘Morocco’ wa Namungo atakuwa na kazi ya kufanya ili kuhakikisha wanaendeleza ushindi kwa kuifunga Yanga ili kujiondoa katika nafasi mbaya waliyopo akitegemea zaidi ubora wa mshambuliaji Reliants Lusajo na kiwango cha kipa Jonathan Nahimana.

“Tumejiandaa kucheza na Yanga, tunafahamu ubora wao lakini pamoja na mwenendo mbaya tumeanza kubadilika ushindi tulioupata dhidi ya Mtibwa umetupa hamasa na tunataka kuendelea kushinda ili kurudisha matumaini ya mashabiki wetu,” alisema Morocco.

Katika mchezo huo Namungo itaendelea kumkosa mshambuliaji wake Bigirimana ambaye ni majeruhi wa muda mrefu, huku Sey akitarajiwa kuanza baada ya kupumzika katika mechi kadhaa zilizopita kutokana na uchovu wa michuano ya kimataifa.

Yanga itawakosa baadhi ya nyota kutokana na sababu mbalimbali akiwemo Car-

linhos, aliyeumia kwenye mchezo uliopita wa Kombe la FA dhidi ya Tanzania Prisons wengine ni Yassin Mustapha na Balama Mapinduzi, ambao ni majeruhi wa muda mrefu.

Uwepo wa Saido Ntibazonkiza, Yacouba Sogne, Michael Sarpong na Feisal Salum vinampa matumaini makubwa kocha Nabi na tayari ametamba kuwa ushindi ni lazima kwa timu yake sababu lengo lao ni kutwaa ubingwa wa ligi simu huu.

“Lengo ni kushinda ingawa wapinzani wetu siyo timu mbaya nimewafuatilia katika mechi za hivi karibuni naamini tunaweza kushinda na tumepanga kucheza kwa kushambulia muda wote wa mchezo,” alisema Nabi.

Nabi anataka ushindi sababu anajua utazidi kumpa matumaini ya ubingwa, lakini endapo watapoteza mchezo huo, Azam itawafikia ambayo tofauti yao ni pointi tatu, hivyo kama watashinda mchezo wao wa leo dhidi ya KMC, wotalingana kwa pointi 57, lakini Azam FC, watakuwa mbele kwa mchezo mmoja.

Mchezo mwingine wa ligi leo ni ule wa Azam FC ambao wataikaribisha KMC katika

uwanja wa Azam Complex Mbande nje kidogo ya Jiji la Dar es Saam.

Huu ni mchezo wa kulipa kisasi kwa wenyeji Azam ambao katika mchezo wa mzunguko wa kwanza walipoteza kwa bao 1-0 bao la Lusajo ambaye sasa ameihama timu hiyo na kurudi Namungo FC.

Kocha George Lwandamina atakuwa na kazi ya kulipa visasi kama alivyofanya kwa Yanga ambayo iliwafunga kwenye mchezo wa kwanza, lakini wakati huo kocha akiwa Mromania Aristica Cioaba.

Lwandamina tangu ameichukua timu hiyo amejitahidi kuibadilisha na kuipa matokeo chanya na sasa Azam imerudi kwenye mbio za ubingwa, hivyo KMC inakazi ya kufanya kuwazuia akina Prince Dube, Idd Seleman ‘Nado’ na wengine ambao wanaweza kuleta madhara kwenye lango lao linalolindwa na kipa mkongwe Juma Kaseja.

“Nawaheshimu KMC ni timu nzuri inacheza kwa muunganiko mzuri kutoka nyuma adi kwenye eneo la mwisho lakini tunacheza nao kwenye uwanja wetu wa nyumbani tuna kila sababu ya

kupata matokeo ukizingatia wachezaji wangu wote wapo fiti,” alisema Lwandamina.

Kwaupande wake kocha Habibu Kondo wa KMC, amekiri kwamba wanakwenda kukutana na timu bora kwenye ligi ya Tanzania, lakini wamejiandaa kucheza nao ili kupata matokeo ingawa anajua haitokuwa kazi rahisi.

Alisema wamejiandaa vizuri kwa ajili ya mchezo huo na watambana kwa dakika zote 90 kuhakikisha wanaifunga Azam na kuweka rekodi ya kuchukua pointi sita dhidi ya waajiri wake wa zamani.

“Tumejipanga vizuri najua utakua mchezo mgumu kwetu na kwao pia lakini tumejiandaa kutoa burudani safi itakayo wapa burudani watazamaji na mwisho wasiku tunazitaka pointi tatu ili kutimiza lengo letu la kumaliza msimu kwenye nne bora msimu huu,” alisema Kondo.

Mchezo wa mwisho utapigwa uwanja wa Jamhuri mkoani Morogoro Mtibwa Sugar watakuwa wenyeji wa Maafande wa Tanzania Prisons, huu ni mchezo mwingine ambao nao unatarajiwa kuwa

na ushindani wa aina yake kutokana na wenyeji Mtibwa Sugar kuwa katika nafasi mbaya ya kushuka daraja msimu huu.

Mtibwa inashika nafasi ya 17 kwenye msimamo ikiwa na pointi 28 katika idadi kama hiyo ya mechi ilizocheza inahitaji kushinda mechi zake zilizo salia wakianzia na mcheo wa leo dhidi ya Tanzania Prisons ili kujinusuru na janga la kushuka daraja vinginevyo mabingwa hao wa ligi kuu msimu wa 1999 na 2000 huenda wasiwepo kwenye ligi ya msimu ujao.

Majanga ya kukimbiwa na kocha Thiery Hitimana na mtangulizi wake Zuber Katwila bado inaonekana kuigarimu timu hiyo ambayo kila kukicha kunafanya kuwaweka katika nafasi ngumu huku kocha wa muda Vicent Barnabas akionekana kuzidiwa mbinu na wapinzani wao.

Tanzania Prisons wapo nafasi ya sita kwenye msimamo baada ya kutolewa na Yanga kwenye michuano ya Kombe la FA, watalazimika kukaza kwenye mechi za ligi zilizosalia ili angalau waweze kumaliza ligi ya msimu huu kwenye nafasi tano za juu.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/75a1123010a536e526b6d9984a9dec92.jpeg

TAASISI ya Mama Ongea ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi