loader
Dstv Habarileo  Mobile
Wateule washukuru Mungu,wasema ni deni kubwa

Wateule washukuru Mungu,wasema ni deni kubwa

VIONGOZI walioteuliwa katika nyadhifa mbalimbali ikiwamo ukuu wa mkoa na taasisi wamezungumzia uteuzi huo wakisema ni deni kubwa kwao kuaminiwa na Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuahidi kutomuangusha.

Mkuu wa Mkoa mteule wa Dar es Salaam, Amos Makalla, amemshukuru Mungu pamoja na Rais Samia kwa kumuamini.

“Niko Mzumbe (Morogoro) huku, sikuwa na taarifa zozote, nafungua simu nakutana na uteuzi. Siwezi kusema sana ila namshukuru Mungu kwa kila jambo, kwa sababu

niliwahi kuambiwa tazama nyuma kwa shukrani, juu kwa imani na mbele kwa matuamini. Namshukuru sana Rais Samia kwa kuniamini, naahidi sitamuangusha,” alisema Makalla.

Katibu wa Bunge mteule, Nenelwa Mwihambi, alisema; “Nimefurahi kuona nimeaminika kushika nafasi hii muhimu. Naahidi kuendelea kuchapa kazi kwa kuzingatia Katiba, sheria, kanuni, miongozo na taratibu zilizopo”.

Mkuu wa Mkoa mteule wa Arusha, David Kafulila alimshukuru Mungu kumtumia Rais Samia na kumuamini akisema, amekopeshwa imani ambayo atailipa kwa kuchapa kazi. “Imani huzaa imani na 

ukiaminiwa ni kama kukopeshwa,” alisema.

Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Geita ambaye sasa ameteuliwa jana kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mara, Robert Gabriel alisema: “Nimeahidi vitu viwili kwa Mungu, uaminifu na matokeo ya kazi. Mungu aliyenifanikisha huku (Geita) hajabadilika, naenda kufanya kazi, Watanzania wanataka maendeleo tena kwa haraka, wamekiamini chama (CCM) na kukipa ridhaa kuunda serikali, nasi lazima tuoneshe huo uaminifu kwa vitendo.”

Alimshukuru Samia na kusisitiza kuwa anajisikia kuheshimiwa na Rais kwa kuona anaweza kufanya kazi na kuleta matokeo chanya.

foto
Mwandishi: Lucy Lyatuu na Evance Ng’ingo

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi