loader
Cantona apewa tuzo ya heshima Ligi Kuu

Cantona apewa tuzo ya heshima Ligi Kuu

GWIJI wa Manchester United Eric Cantona amekuwa wa tatu kupata tuzo ya heshima ya Ligi Kuu baada ya Thierry Henry na Alan Shearer.

Cantona, 54, alijiunga na United akitokea Leeds United mwaka 1992 na kuwa mmoja wa wachezaji maarufu zaidi klabuni hapo, akishinda mataji manne ndani ya misimu mitano wakati huo kikosi kikiwa chini ya Alex Ferguson na kikitawala Ligi Kuu.

“Nina furaha sana na najivunia, lakini pia sijashangazwa sana,” alisema Cantona kwenye taarifa yake jana. “Ningeshangazwa kama nisingechaguliwa.”

“Nimekuwa mwenye bahati kucheza kwenye timu hii, nikiwa na wachezaji wazuri, kocha na mashabiki wema, tulishinda na ilikuwa ni soka niliyoiota kwasababu Manchester United ilikuwa klabu iliyotaka kushinda mataji.”

Mbali na kushinda mataji manne ya Ligi Kuu, Cantona alifunga mabao 70 katika mechi 156 alizocheza, pia alitoa pasi 56 za mabao kabla ya kustaafu mwaka 1997 akiwa

na umri wa miaka 30.

Akizungumzia maisha yake alisema moja ya tukio alipendalo lilikuwa ni kushinda taji kwa mara ya kwanza akiwa na United. Ilitwaa taji hilo baada ya miaka 26.

“Baada ya miaka 26, Manchester United hatimae ilishinda taji lake la kwanza la ligi na ilikuwa ni mwaka wangu wa kwanza kwenye Ligi Kuu pia,” aliongeza.

“Nimekuwa mwenye bahati kucheza timu hii ikiwa na wachezaji wazuri, kocha mzuri na mashabiki wazuri, nilikuwa naota hilo siku zote, nilipokuwa mdogo nilikulia Holland na Ajax Amsterdam katika kizazi cha Johann Cruyff. Ilikuwa ni soka tu, soka iliyohamasisha.”

“Nimekuwa mwenye bahati kucheza Manchester United kwa sababu tulicheza soka safi na tulishinda mataji.

Tulifanya kazi kwa bidii, kwa bidii sana, usisahau kwamba tulifanya kazi kwa bidii na kwa kujiamini, tulifurahia na kucheza soka safi.”

Kustaafu kwake akiwa na umri wa miaka 30 kulishangaza wengi na tangu wakati huo alisema amepoteza mapenzi yake na soka.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/c805d9276318eebdc13881e3a2e8278d.png

MWENGE wa Uhuru unaendelea ...

foto
Mwandishi: MANCHESTER, England

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi