loader
Dstv Habarileo  Mobile
Benzema aitwa kikosi cha Ufaransa

Benzema aitwa kikosi cha Ufaransa

MSHAMBULIAJI  wa Real Madrid Karim Benzema yumo katika orodha ya wachezaji 26 watakaounda kikosi cha timu ya taifa ya Ufaransa kwa ajili ya michuano ya Mataifa ya Ulaya baada ya kutokuwemo kwa takribani miaka sita.

Hajaichezea nchi yake tangu mwaka 2015 kutokana na madai ya kujihusisha na kutuhumiwa kujihusisha na kesi ya usaliti iliyokuwa ikimuhusu mchezaji mwenzake wa Ufaransa.

Benzema, 33, alikosa kampeni ya Ufaransa kucheza michuano ya Euro 2016 na hakuwemo wakati timu hiyo ikishinda taji la Dunia mwaka 2018 kutokana na tuhuma hizo.

Januari mwaka 2021 muendesha mashtaka wa Ufaransa alitangaza kuwa,  Benzema atakabiliwa na mashatka.

Anadaiwa kumlipa mtu mmoja ili kuchukua fedha kutoka kwa kiungo Mathieu Valbuena, 36, kwa kutishia kusambaza hadharani picha zake za video za ngono mwaka 2015, lakini mshambuliaji huyo alisema ofisa wa polisi hakutumia utaratibu mzuri katika suala hilo.

Baada ya kuthibitisha, Benzema yuko katika kikosi, kocha wa Ufaransa Didier Deschamps alisema: "Kitu muhimu sana ni leo na kesho.

"Kulikuwa na hatua muhimu. Tulionana wote. Tulizungumza kwa kirefu. ..Sikutoa hadharani neno lolote kuhusu mjadala wetu. Alihitaji, nilihitaji hilo.”

Hugo Lloris na Moussa Sissoko wa Tottenham Hotspur, beki wa kushoto wa Everton Lucas Digne, mchezaji wa Chelsea Kurt Zouma, Olivier Giroud na  N'Golo Kante na Paul Pogba wa Manchester United wote wamo katika kikosi hicho cha Ufaransa.

Euro 2020 – Kundi F

Hungary, Ureno, Ufaransa, Ujerumani

Benzema alifunga mabao 27 katika mechi 81 alizoichezea Ufaransa, ikiwemo kuifungia mara mbili katika mechi mbili alizoichezea timu ya taifa kwa mara ya mwisho waliposhinda 4-0 mchezo wa kirafiki dhidi ya Armenia.

Ni mmoja wa wachezaji muhimu wa Real Madrid msimu huu, alifunga mabao 29, yakiwemo 11 katika mechi 10 na alisaidia mara nane katika mashindano yote.

Vigogo hao wa Hispania wanania ya kuwapiku vinara wa La Liga Atletico Madrid na kuweka rekodi ya kutwaa taji hilo kwa mara ya 35 wakati umebaki mchezo mmoja.

Ufaransa itaanza kampeni zake za Euro 2020 kwa kucheza dhidi ya Ujerumani Juni 15.

Kikosi cha Ufaransa:

Makipa: Hugo Lloris (Tottenham), Mike Maignan (Losc) na Steve Mandanda (Marseille)

Mabeki: Lucas Digne (Everton), Leo Dubois (Lyon), Lucas Hernandez (Bayern Munich), Presnel Kimpembe (PSG), Jules Kounde (Sevilla), Clement Lenglet (Barcelona), Benjamin Pavard (Bayern Munich), Raphael Varane (Real Madrid) na Kurt Zouma (Chelsea)

Viungo: N'Golo Kante (Chelsea), Thomas Lemar (Atletico Madrid), Paul Pogba (Manchester United), Adrien Rabiot (Juventus), Moussa Sissoko (Tottenham) na Corentin Tolisso (Bayern Munich)

Washambuliaji: Wissam Ben Yedder (Monaco), Karim Benzema (Real Madrid), Kingsley Coman (Bayern Munich), Ousmane Dembele (Barcelona), Olivier Giroud (Chelsea), Antoine Griezmann (Barcelona), Kylian Mbappe (PSG) na Marcus Thuram (Borussia Monchengladbach)

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/7eea06e9116149916262607ca966f68b.jpeg

BAADA ya Yanga kuondolewa kwenye michuano ya Ligi ...

foto
Mwandishi: MADRID, Hispania

1 Comments

  • avatar
    Mussa nyabulo
    20/05/2021

    Franch be come a champion

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi