loader
Azam wapania taji la Ligi Kuu 

Azam wapania taji la Ligi Kuu 

BAADA ya kupata ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Biashara United, Kocha  Mkuu wa timu ya Azam FC, raia wa Zambia  George Lwandamina,  amesema kuwa bado yuko katika mbio za ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara licha ya kuzidiwa pointi moja  na vinara Simba na Yanga.

Azam walipata mabao yao kupitia kwa mshambuliaji kiongozi  Prince Dube, katika dakika ya 11 huku wakiongeza la pili katika dakika ya 54 kupitia kwa kiungo Mudathir Yahya .

Ushindi huo umeifanya Azam FC kufikisha pointi 60 baada ya michezo 30 lakini ikiendelea kusalia  katika nafasi ya tatu katika msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, pointi moja nyuma ya Simba na Yanga, ambao kila mmoja ana pointi 61.

Akizungumza na gazeti hili baada ya mchezo huo,  Lwandamina  alisema  kuwa amefurahishwa na matokeo hayo, ambayo wameyapata katika mchezo huo yamewaongezea kasi katika mbio za kulisaka taji la Ligi Kuu  Tanzania Bara.

“Ulikuwa mchezo muhimu kwetu katika mbio za ubingwa nashukuru tumepata matokeo mbele ya timu bora tulikuwa vizuri kila idara  tulitengeneza nafasi, ambazo tumezitumia kupata matokeo,” alisema Lwandamina.

Naye Kocha Mkuu wa timu ya Biashara United, Patrick Odhiambo, alisema kuwa mchezo ulikuwa mzuri wameadhibiwa kutokana na makosa waliyofanya, lakini hiyo haiwezi kuwafanya wakakata tamaa katika mipango yao ya michezo ijayo ya Ligi Kuu ya Tanzania Bara.

“Nawapongeza wapinzani wetu walikuwa bora ndio maana wamepata matokeo tunarudi kujipanga kurekebisha tulipokosea ili tusirudie makosa katika michezo inayofuata,” alisema Odhiambo.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/a9838c80fe999d8ea525eae16084862d.jpeg

TAASISI ya Mama Ongea ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi