loader
Dstv Habarileo  Mobile
Man City, Chelsea vita ya tatu

Man City, Chelsea vita ya tatu

MACHO ya wapenzi wa  soka duniani leo yatakuwa kwenye uwanja wa Estadio do Dragao Ureno itakapopigwa fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kati ya miamba ya England, Manchester City na Chelsea. 

Miamba hiyo ambayo imekuwa katika kiwango bora msimu huu inaenda kuandika historia wakati Man City wakisaka taji lao la kwanza la Ligi ya Mabingwa,  Chelsea wao watakuwa wakihitaji kuongeza kombe la pili baada ya lile walilotwaa mwaka 2012 Ujerumani.

Man City wamekuwa katika kiwango bora chini ya Pep Guardiola msimu huu tayari wametwaa mataji mawili la  Ligi Kuu England na kombe la ligi, wanaingia katika mchezo huu wakiwa na morali ya hali ya juu.

Upande wa Chelsea wakiwa chini ya Thomas Tuchel, wanaingia katika mchezo huo wakiwa na presha kubwa baada ya kumaliza nje ya nafasi nne za juu katika msimamo wa Ligi Kuu ya England, lakini wakiwa na kumbukumbu nzuri ya kuibuka na ushindi dhidi ya City katika mchezo wa Ligi Kuu ya England.

Huu unakuwa mchezo wa 169 kuzikutanisha timu hizi katika mashindano yote ambapo katika michezo 168, Chelsea ni wababe  wakiwa wameshinda mara 70, huku Man City wakiwa wameshinda mara 59 na kutoka sare mara 40.

Katika mchezo wa mwisho wa kuikutanisha miamba hiyo  miwili, Chelsea waliondoka kifua mbele kwa kuibuka na ushindi wa mabao 2-1, lakini pia iliwafurusha matajiri hao wa jiji la Manchester katika michuano ya FA.

Kocha Mkuu wa Man City,  Guardiola, amesema kutakuwa na mabadiliko mengi ya kushangaza katika orodha ya wachezaji watakaoanza katika kikosi chake kwani ni jambo la kuvutia mosi atauangalia mchezo kama shabiki wa Man City, kisha atakaa na kuuchambua.

“Katika michezo tuliyokutana Ujerumani ilikuwa ya kuvutia lakini migumu kwani mpinzani wangu Tuchel ni mtu wa mipango, lakini sasa kila timu imebadili staili ya uchezaji mara mbili au tatu  ni sawa na kucheza Chess,” alisema Guardiola.

Naye kocha wa Chelsea,Tuchel, alisema kuwa anajua  Pep yuko vizuri Manchester City ameonesha kitu kizuri  England, lakini mchezo utakuwa wazi kwa timu zote.

“Baada ya kuumia katika mchezo uliopita dhidi ya Aston Villa, mlinda mlango Edouard Mendy, anarejea tena langoni lakini bado nina wasiwasi na hali ya kiungo wangu  N’Golo Kante ambaye hali yake ilikuwa bado haijatengamaa,” alisema Tuchel.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/904640646138182b1e6747940fca61bf.jpeg

OLE Gunnar Solskjaer amesema, kuwasili kwa ...

foto
Mwandishi: LISBON, URENO

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi