loader
Dstv Habarileo  Mobile
Watendaji kubanwa fedha zinazobaki halmashauri

Watendaji kubanwa fedha zinazobaki halmashauri

SERIKALI imeiagiza Wizara ya Fedha na Mipango kubadili kanuni ili kuruhusu fedha zilizobaki katika halmashauri kuendelea kutumika kwa miezi kadhaa baada ya mwaka wa fedha kukamilika ili kukamilisha miradi ya maendeleo.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alitoa agizo hili jana bungeni Dodoma na akabainisha kuwa mabadiliko hayo hayataruhusu au kutoa mwanya kwa watendaji wazembe wanaochelewesha fedha makusudi.

"Wengine watazembea na kukaa na fedha hizo hata miaka miwili, hao watawekewa kifungu cha kuwabana na watachukuliwa hatua kali.”

“Serikali inafanya maboresho hayo, lakini wakurugenzi watatakiwa kuandika barua kueleza kwa nini wamechelewa kutumia fedha hizo katika muda uliopangwa,” alisema Majaliwa.

Alisema serikali itafanya marekebisho na itatoa taarifa bungeni ili wabunge wayafahamu marekebisho hayo.

Majaliwa alikuwa bungeni alipojibu mwaswali ya wavubge likiwampo la Mbunge wa Singida Mashariki, Elibariki Kingu (CCM), katika Kipindi cha Maswali ya Papo hapo kwa Waziri Mkuu.

Kingu alitaka kufahamu kwa nini serikali inarudisha fedha Hazina zinapokuwa zimetolewa mwishoni mwa mwaka wa fedha na hivy,o kusababisha miradi mingi kukwakama.

Majaliwa alisemaSserikali ya Awamu ya Sita imeweka utaratibu wa kupeleka fedha kutekeleza miradi katika halmashauri mwanzoni na mwisho mwa mwaka wa fedha.

Alisema serikali iliweka sheria ya kurudisha fedha Hazina baada ya mwaka wa fedha kukamilika na halmashauri inatakiwa kuandika barua kwa nini haijazitumia.

foto
Mwandishi: Magnus Mahenge, Dodoma

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi