loader
NJE YA CHAKI

NJE YA CHAKI

*Ngolo analitendea haki jina
WIKI iliyopita tulishuhudia Klabu ya Chelsea wakitwaa taji la Ligi ya Mabingwa wa Ulaya mbele ya Manchester City baada ya kuwafunga bao 1-0 katika mchezo uliofanyika Porto, Ureno.

Gumzo kubwa limekuwa juu ya kiwango bora kilichooneshwa na kiungo wa mabinbwa hao, matajiri wa jiji la London, mfaransa Ngolo Kante.

Wachambuzi na watu wa takwimu wamebainisha kuwa ubingwa wa Chelsea umechangiwa kwa kiasi kikubwa na kazi nzuri iliyofanywa na Kante kwa kuhakikisha anakuwa kiunganishi bora wa mipira kutoka kwenye safu ya ulinzi kwenda kwa washambuliaji na pia kupoozesha mashambulizi yasiwe hatari kwa safu yake ya ulinzi.

Ukimuangalia uwanjani au hata nje ya uwanja utabaini si mtu wa kupenda makuu, lakini takwimu zake za ndani ya uwanja zinakupa taswira halisi yakuwa jamaa huyu ni mpambanaji haswa.

Waswahili husema jina huumba, hii inadhihirika kabisa kwa Kante ambaye makubwa anayoyafanya yanatokana na jina lake alilopewa na wazazi wake.

Jamaa huyu ni mwenye asili ya Mali kwa sasa pasi yake ya kusafiria inaonesha ni Mfaransa baada ya kuamua kuchukua uraia wa nchi aliyozaliwa, wazazi wake walihama kutoka Mali na kwenda Ufaransa mwaka 1980.

Baba yake alimpa jina la Ngolo kumuenzi mfalme aitwaye Ngolo Diarra ambaye alikuwa akiitawala himaya ya Bamana enzi hizo iliyokuwepo katika nchi ya Mali.

Baba yake ambaye alifariki dunia wakati Kante akiwa na umri wa miaka 11 tu, aliamua kumpa jina hilo akiamini kuwa mwanawe ataweza kuja kuwa mtu mpambanaji na kuongoza vema katika nafasi, ambayo atawekwa au kuifanyia kazi.

 Awali Kante hakupenda kabisa kucheza mpira wa nguvu, kukabana kutokana na kwamba alikiuwa akivutiwa mno na uchezaji wa Diego Maradona, Ronaldinho na Christiano Ronaldo, lakini akajikuta akipangwa kiungo mkabaji ndipo anacheza kwa umakini zaidi.

Usione kama Kante anavyovifanya uwanjani anabahatisha, bali ni mtu wa mahesabu, wasawahili tunasema hesabu zimelala kichwani, tambua kuwa alishakaa darasani na kuchukua diploma ya uhasibu.

Rafiki zake wakaribu wanamuelezea kuwa jamaa hapendi maisha ya kujionesha ni msiri sana katika mambo yake.

Licha ya wachezaji wenzake kupenda anasa, lakini yeye hayupo hivyo usafiri wake mkubwa akiwa Ufaransa ni pikipiki na alipokwenda Uingeteza aliamua kununua gari dogo la milango mitatu, ambalo hutumiwa mno na watu wa hali ya chini.

Mbali na soka anapenda pia kucheza tenisi na pia anaependa nyimbo za karaoke ambazo anasema humburudisha sana kwakuwa zinapigwa vizuri, tofauti na mitindo mingine ya muziki, chakula anachokipenda ni mchanganyiko wa wali, samaki na nyama, mlo unaopendwa mno na watu wa Afrika Magharibi.

 

https://www.apps.tsn.go.tz/public/uploads/044bd0f4a04f997cce4b19f23170d331.jpeg

NIPO nyumbani kwa Baba na Mama Chichi. ...

foto
Mwandishi: Mohammed Mdose

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi