loader
Dstv Habarileo  Mobile
Wachezaji kuweni makini usajili 2021/22

Wachezaji kuweni makini usajili 2021/22

LIGI Kuu ya Tanzania inaelekea ukingoni huku kila timu ikiangalia na kufanya tathimini ya kile ilichovuna kuanzia mwanzo wa mashindano hadi walipofika hivi sasa kama imefikia malengo au wamekwama.

Ikiwa wamefikia malengo ni jambo la kheri lakini kama wamefeli waangalie wapi walipojikwaa na kurekebisha baadhi makosa waliyofanya ili yasijirudie katika msimu ujao wa ligi.

Wakati huu ligi ikielekea ukingoni timu zimeanza kuimarisha vikosi vyao kama kufanya sajili za wachezaji wapya ili tu kuimarisha mabenchi yao ya ufundi kwaajili ya msimu unaokuja wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara.

Sio kwamba dirisha la usajili limefunguliwa la hasha bali ni kutokana na baadhi ya wachezaji ambao kandarasi zao zimefika mwishoni au walio na mikataba chini ya miezi sita ambao kikanuni wanaruhusiwa kufanya mazungumzo na timu nyingine.

Katika madirisha ya usajili mara nyingi kumekuwa na utata hasa kwa wachezaji kusaini timu zaidi ya moja tuliwahi kuona kwa nyota kama winga Mrisho Ngasa mwaka 2013 wakati akijua fika ana mkataba na Azam Fc alisaini mkataba wa siri na Yanga jambo lililomfanya apigwe faini ya Sh milioni 45 kwa kosa hilo.

Kiungo mshambuliaji Mohamed Mkopi mwaka 2016 alijikuta akikaa nje ya Uwanja mwaka mzima baada ya kusaini timu mbili wakati akijua fika bado hajamalizana na waajiri wake Tanzania Prisons, akasaini kwa watani wao wa jadi Mbeya City jambo lililomfanya akutane na rungu hilo.

Pius Buswita, ambaye alidumu katika kikosi cha Yanga kwa miaka miwili wakati anaondoka Mbao aliingia kandarasi na Simba lakini baadaye akasaini Yanga, jambo ambalo likamfanya apitiwe na rungu la kufungiwa na kutakiwa kurudisha fedha za Simba.

Naye kiungo wa zamani wa Kagera Sugar, Ludovic Venance mwaka 2017 alipitiwa na rungu baada ya kusaini mkataba mpya na African Lyon, wakati akijua fika kuwa bado ni mwajiriwa wa Mbao FC, ambapo alijikuta akikosa michezo minne ya timu yake mpya.

Sakata kama hili pia limetokea msimu wa 2020/21 ambapo kiungo Benard Morrison, amesaini kandarasi na Simba wakati klabu ya Yanga ikidai kuwa ina mkataba na mchezaji huyo ambapo hadi sasa kesi ya wawili inaendelea katika mahakama ya usuluhishi CAS.

Wakati tukisubiri Shirikisho la mpira wa miguu hapa nchini kutangaza tarehe ya ufunguzi wa dirisha la usajili nataka kutoa rai kwa wachezaji pamoja na klabu kuwa makini kipindi hiki ili kukwepa kukutana na adhabu za kufungiwa na kulipishwa faini kwa kosa ambalo limekuwa likijirudia misimu nenda rudi.

Naamini timu pamoja na wachezaji watajifunza kupitia kwa mifano hii ambayo iko wazi ili kulinda taswira ya Ligi Kuu Tanzania Bara pamoja na wao katika jamii ya wapenda soka.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/c64d92ab7c0e46d28a4d4a337141969c.png

LEO katika mwendelezo wa makala za ...

foto
Mwandishi: Martin Mazugwa

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi