loader
Dstv Habarileo  Mobile
Waliokopa na kutelekeza mashamba 16 kukiona

Waliokopa na kutelekeza mashamba 16 kukiona

WAZIRI wa Kilimo, Profesa Adolf Mkenda amesema serikali haitawavumilia wawekezaji waliochukua mikopo na kutelekeza mashamba 16 ya maua na mboga mboga wilayani Arumeru mkoani Arusha.
Profesa Mkenda alisema hayo mwishoni mwa wiki alipokagua mashamba yenye ukubwa wa ekari 1,950 wilayani humo na akasema wawekezaji hao walichukua mikopo na hawakurudisha hivyo kuisababishia serikali hasara tangu mwaka 2018.

Kwa mujibu wa profesa Mkenda mashamba hayo kwa mwaka mmoja yanapoteza zaidi ya Dola za Marekani milioni 24 sawa na ajira 6,700 kwa mwaka.

"Serikali itahakikisha mashamba hayo yanarudi katika hali yake ya uzalishaji huku taratibu nyingine za kurejesha mikopo hiyo ikiendelea" alisema na kuongeza;

"Mashamba haya ya maua yamefungwa kutokana na wawekezaji waliochukua mikopo ya kimagumashi, mashamba haya yametelekezwa na yanaharibika wakati nchi hii tunahitaji fedha za kigeni na ajira kwa wananchi wetu, hivyo hatutamvumilia wala kumtetea aliyechukua mkopo kimagumashi"

Profesa Mkenda alisema ni vigumu kuamini kampuni iliyokuwa ikifanya biashara vizuri ingechukua mkopo na isiendeleze mashamba hayo.

"Lazima kuna mchezo ulifanyika baina ya aliyetoa mkopo na aliyepokea mkopo," alisema na kuongeza;

"Wizara tunaenda kujenga hoja ili haya mashamba yaliyotelekezwa yanarudi katika hali yake ya kawaida ya uzalishaji na kama kuna wawekezaji wengine tuwape wayaendeleze,"

Mkurugenzi Mtendaji wa Chama Cha Wakulima wa Mbogamboga na Matunda Tanzania (TAHA), Dk Jacqueline Mkindi alisema kutelekezwa mashamba hayo kumepoteza zaidi ya ajira 6,700 za Watanzania na kuisababishia serikali hasara.

Dk Mkindi alisema mashamba hayo yalikuwa yakiuza maua na bidhaa nyingine kwenye masoko ya kimataifa na ameomba serikali ione namna ya kuyarejesha yafanye kazi ili yaongeze pato la taifa na ajira kwa Watanzania.

https://www.apps.tsn.go.tz/public/uploads/68759e866635281a8cbe4228e6166f0d.jpeg

WIZARA ya Kilimo imesema Desemba mwaka huu ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Maalumu, Arusha

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi