loader
Dstv Habarileo  Mobile
Same, Mwanga wataka elimu ya kukabiana na wanyama

Same, Mwanga wataka elimu ya kukabiana na wanyama

WAKAZI wa wilaya za Same na Mwanga hususani waishio karibu na maeneo ya mapito ya wanyama wamesema wanahitaji elimu ya ziada ya kukabiliana na wanyama wakiwamo tembo ambao wanafahamu ratiba ya siku za soko katika wilaya hizo na kuvamia.

Wakazi wa wilaya hizo wamekuwa wakisumbuliwa na tembo kutoka Hifadhi ya Tsavo nchini Kenya na Mkomazi nchini na mtu mmoja amekufa baada ya kushambuliwa na wanyama hao, huku zaidi ya ekari 600 za mazao zikiharibiwa.

Wananchi hao walisema tembo ambao ni mnyama wenye akili kuliko wote duniani, wanafahamu ratiba ya siku za soko za Alhamisi na Jumapili wilayani Same ambapo huvamia na kula mazao na bidhaa nyingine zinazopelekwa masokoni.

Ofisa Wanyamapori Mkuu kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii, Anthonia Rafael alisema serikali inatambua tatizo hilo na imeanzisha mpango wa kutoa elimu kwa mwaka 2020/2024 ambapo wananchi wanaelimishwa namna ya kuwakabili wanyama bila kuwaua.

"Tayari mafunzo yametolewa mkoa wa Simiyu, Ruvuma, Morogoro na sasa Kilimanjaro ikiwa ni utekelezaji wa mkakati wa kitaifa wa kusimamia utatuzi wa migongano ya wanyama na binadamu kuepusha athari," alisema.

Mtafiti wanyamapori kutoka Taasisi ya Wanyamapori Tanzania (Tawiri), Dk Emmanuel Asenga alisema mbinu za kuwadhibiti wanyama pori zinatumika pia kimataifa ili kupunguza athari kwa binadamu na mazao.

"Tumetumia mbinu kama oil chafu, tofali za pilipili, uzio wa pilipili na bomu la asili la kutupa kwa mkono lililotengenezwa na honi, fataki, na mchanga, pia kuna mbinu nyingine za kupiga madebe ili kufukuza wanyama hao," alisema.

Kuhusu kuuzwa ghali kwa vifaa vya kudhibiti tembo kama vile tochi zenye mwanga mkali, alisema serikali imejipanga kuhakikisha bei za bidhaa hizo zinapungua.

Wakazi wa kijiji cha Mheza, kata ya Maore, wilaya ya Same, Asha Omary na Zena Juma  waliiomba kubadilishiwa mbinu za kudhibiti wanyama hao mara kwa mara kwani ni rahisi kwa tembo kubaini mbinu zinazotumika.

Wataalamu wa wanyama pori wanasema tembo wana akili nyingi kuliko mnyama yeyote wa nchi kavu, ana uwezo wa kujua majani ya dawa kuanzisha uchungu wa kuzaa, kutambua vitu kwenye kioo, kuigiza sauti mbalimbali na kutumia vitu mbalimbali kwa matumizi sahihi pasipo kufundishwa na  wanyama pekee wanaoweka msiba pale mwenzao anapokufa.

https://www.apps.tsn.go.tz/public/uploads/b2af1557160ff6e60245bb1bdf6513de.jpeg

ALIYEKUWA Mbunge Mteule wa Jimbo la Konde ...

foto
Mwandishi: Nakajumo James, Same

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi