loader
Dstv Habarileo  Mobile
Matukio zaidi ya 36,000 ya ukatili kwa watoto yaripotiwa

Matukio zaidi ya 36,000 ya ukatili kwa watoto yaripotiwa

JUMLA ya makosa 36,940 ya ukatili wa kingono, ubakaji na ulawiti watoto yameripotiwa katika vituo vya polisi nchini katika kipindi cha miaka mitano iliyopita.

Mkoa wa Kigoma umetajwa kuwa miongoni mwa mikoa 10 inayoongoza kwa ukatili wa kingono kwa watoto.

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Jukwaa la Utu wa Mtoto (CDF), Koshuma Mtengeti alisema hayo juzi kwa nyakati tofauti wakati wa kukabidhi madawati  ya jinsia na watoto kwa Jeshi la Polisi katika wilaya za Buhigwe na Uvinza yaliyojengwa kwa ufadhili wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya ya Uzazi (UNFPA).

Alisema pamoja na kuwapo kwa matukio mengi ya ukatili kwa wanawake na watoto,  wahusika ambao sehemu kubwa ni ndugu wa karibu wa familia za waathirika hawajachukulia hatua stahili za kisheria na kesi nyingi kufutwa kutokana na kukosa ushahidi.

Aidha, alisema mwaka jana  pekee, matukio 26,544 ya ukatili dhidi ya wanawake yaliripotiwa katika vituo vya polisi nchini, ambapo 45 katika mikoa 13 yalitolewa hukumu na mahakama.

Alitoa wito kwa wadau wote wanaotetea haki za wanawake na watoto, vyombo vya sheria na wananchi kushirikiana kuhakikisha watuhumiwa wa matukio ya ukatili na  unyanyasaji kijinsia wanafikishwa kwenye vyombo vya sheria na hukumu dhidi yao zinatolewa kwa haki.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Thobias Andengenye aliwataka wanaohusika na masuala ya ukatili dhidi ya watoto kutosubiri malalamiko wakiwa ofisini pekee, bali watoke kwa ajili ya kutoa elimu kwa jamii.

“Kwa siku za karibuni takwimu za makosa hayo zitaongezeka maradufu pamoja na elimu na uhamasishaji jamii unaofanyika, takwimu hizo zitumike kutengeneza mipango ambayo itasaidia kukabiliana na matatizo hayo kwenye jamii,” alisema.

Mkuu wa Kamisheni ya Ushirikishwaji Jamii wa Jeshi la Polisi, Musa Ally alisema kazi ya kudhibiti ukatili na unyanyasaji kijinsia inahitaji nguvu kubwa na ushirikiano wa wadau mbalimbali kutokana na takwimu kuonesha kuongezeka kwa vitendo hivyo.

https://www.apps.tsn.go.tz/public/uploads/4eb4bfae0fdbc6fcd0e502fb18584cb2.jpeg

ALIYEKUWA Mbunge Mteule wa Jimbo la Konde ...

foto
Mwandishi: Fadhili Abdallah, Kigoma

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi