loader
Dstv Habarileo  Mobile
DC: TRA kadirieni kodi kwa haki

DC: TRA kadirieni kodi kwa haki

MKUU wa Wilaya (DC) ya Busega, Tano Mwera, ameitaka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) katika Mkoa wa Simiyu kuwakadiria kodi wafanyabiashara kulingana na viwango na mitaji halisi ya biashara zao.

Amewaagiza pia kuwafanyia makadirio hayo katika maeneo husika ya biashara hizo ili kodi watakazozikadiria ziendane na mitaji.

Alitoa maagizo hayo katika uzinduzi wa ofisi ya TRA wilayani Busega uliofanyika katika Kata ya Lamadi.

Alisema kumekuwepo na malalamiko kutoka kwa wafanyabiashara wilayani humo kuwa mamlaka hiyo haifanyi makadirio halisi kulingana na mitaji waliyowekeza katika biashara zao, badala yake wamekuwa wakipangiwa kulipa kiasi kikubwa.

"Naamini TRA ikifanya makadirio kwa kuangalia mitaji ya wafanyabiashara hao, malalamiko yatapungua sana hivyo nishauri mamlaka hiyo kufanya kazi hiyo kwa kufuata haki," alisema.

Akisoma taarifa ya mamlaka hiyo, Meneja wa TRA Mkoa wa Simiyu, Charles Mkubwa, alisema kwa kuthamini mchango wa wateja wao, wameamua kuwasogezea huduma hiyo karibu ili kuwapunguzia adha ya kufuata huduma hiyo makao makuu ya mkoa kwa zaidi ya kilometa 150.

Mkubwa aliwahakikishia ushirikiano wafanyabiashara wilayani humo na kwamba, ofisi hiyo ya Lamadi itatoa huduma ya usajili wa biashara, ukadiriaji wa kodi, ankara na leseni za biashara.

https://www.apps.tsn.go.tz/public/uploads/8b66bf777754811dfb218ca4c97df875.jpeg

ALIYEKUWA Mbunge Mteule wa Jimbo la Konde ...

foto
Mwandishi: Happy Mollel, Busega

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi