loader
Dstv Habarileo  Mobile
China yatoa onyo kwa G7

China yatoa onyo kwa G7

CHINA imezionya nchi tajiri duniani zinaounda umoja wa G7 ikisema kipindi cha nchi chache kuamua azma ya mwelekeo wa dunia nzima kimekwisha muda mrefu uliopita.

China imetoa kauli hiyo kupitia msemaji wake nchini Uingereza zikiwa ni siku chache tangu wakuu wa mataifa hayo makubwa kukutana Uingereza kufanya mkutano wao wa kila mwaka huku miongoni mwa masuala ya kujadili, ikiwa ni pamoja na mabadiliko ya tabianchi na ushiriki wa China katika umoja huo.

Wachambuzi wa uchumi wa Marekani wamebainisha kuwa, serikali ya Rais Joe Biden imeonesha nia ya kushirikisha mataifa mengine kudhibiti ukuaji wa China.

Kikao hicho kimelenga kuja na maadhimio ili kuzisaidia nchi zinazoendelea zilizokumbwa na changamoto za mabadiliko ya tabianchi ikiwa pamoja na kuendeleza miradi ya miundombinu ambayo imekuwa ikifadhiliwa na China.

Miradi hiyo ya miundombini inakuja kuwa mbadala wa miradi kama hiyo iliyokuwa ikiendeshwa na China ya ujenzi wa barabara, reli za kisasa na hata bandari ambao umeishia kuwa mzigo wa madeni kwa nchi zinazoendelea.

Nia hiyo ndiyo imemwibua Msemaji wa China nchini Uingereza kutoa kauli ya kuwa si tena muda wa nchi hizo za G7 kuendelea kupanga mambo kwa niaba ya dunia nzima.

Msemaji huyo alisema kuwa China inaamini kuwa nchi zote kubwa, ndogo, zenye nguvu na zisizokuwa na nguvu za kiuchumi kuwa zote ni sawa na kuwa masuala yanayohusiana na  mustakabali wa dunia yanapaswa kuangaliwa na kuzingatiwa kutokana na katiba na miongozo sawa.

Juzi G7 ilibainisha kuwa mkutano wa wakuu hao wa nchi utatoa mwongozo kuhusiana na nia na mbinu zao watakazozitumiakatika kufadhili miradi ya maendeleo hasa miundombinu kwa kuzingatia uwazi ili kuondoa uwezekano wa kuja kudhulumiwa rasilimali za nchi.

https://www.apps.tsn.go.tz/public/uploads/1ad0e0825027dbbfb5ef1dc859ccd08c.jpeg

MZOZO umeibuka nchini Somalia juu ...

foto
Mwandishi: LONDON, England

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi