loader
Dstv Habarileo  Mobile
Waitara asimamisha vivuko vya kampuni ya Kamanga

Waitara asimamisha vivuko vya kampuni ya Kamanga

NAIBU Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mwita Waitara, amesimamisha huduma za vivuko viwili vinavyomilikiwa na kampuni ya Kamanga Ferry Limited hadi vitakaporekebisha kasoro zilizobainika.

Alikuwa ameongozana na wadau wengine wa usafirishaji mkoani hapa mwishoni mwa wiki, wakiwemo wa Kampuni ya Huduma za Meli (MSCL), Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) na Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroads).

Waitara alitembelea bandari ya vivuko hivyo (Kamanga Ferry) baada ya Shirika la Uwakala wa Meli (TASAC) kutoa taarifa ya ukaguzi na kasoro zilizobainika katika vivuko hivo.

Waitara na timu yake walikutana na Meneja wa kampuni ya Kamanga, Faustine Elikana, aliyekiri ukaguzi kufanyika na kubaini baadhi ya changamoto alizodai tayari zimerekebishwa, hivyo vivuko hivyo MV Orion na MV Thor, kuendelea na safari zake katika Ziwa Victoria.

Hata hivyo, Naibu Waziri Waitara alionesha kutoridhishwa na hali hiyo ambapo baada ya kukaa kikao cha faragha na wahusika kwa takribani saa mbili, alisema: "Kawaida ni lazima mkaguzi aliyegundua kasoro ajiridhishe na marekebisho yaliyofanyika ndipo safari zianze upya.”

Akaongeza: “Sasa naamuru vivuko hivi visimame kuanzia kesho (Jumamosi) hadi ukarabati ufanyike. Muwatangazie wananchi wajue kusitishwa kwa safari zenu ili wasisumbuke."

Akieleza kilichobainika katika ukaguzi, Meneja wa Mafunzo na Usajili wa Mabaharia TASAC, Iroga Nashon, alisema ni pamoja na uchakavu katika mitambo ikiwemo injini na jenereta.

Alisema wakala ulimtaka pia mmiliki kutafuta cherezo na kupandisha vivuko juu ili wataalamu wavikague chini kujua kama pako salama, lakini hilo halikufanyika.

Nashon alieleza zaidi kwamba mmiliki alielekezwa pia na wakala kufunga kifaa maalumu cha kupima kina cha maji 'Echo Sounder' ili kutambua kama vivuko viko sehemu salama, lakini hilo pia halikufanyika.

"Tulikuta matangi ya maji nayo yamechakaa. Tulibaini kasoro nyingi, lakini nyingine ni za kitaalamu zaidi ambazo nashindwa hata namna ya kuziweka ila mzielewe ipasavyo na hivyo, tukaagiza vivuko kusimama tangu Mei 26, lakini hakuna agizo lolote lililotekelezwa hadi Naibu Waziri alipoingilia kati," alisema.

https://www.apps.tsn.go.tz/public/uploads/1bbb1f51806c2c349411652b2057b397.jpeg

ALIYEKUWA Mbunge Mteule wa Jimbo la Konde ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu, Mwanza

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi