loader
Dstv Habarileo  Mobile
U-20 Yanga, Simba zashikana kileleni

U-20 Yanga, Simba zashikana kileleni

HATUA ya nane bora ya Ligi ya vijana chini ya umri wa miaka 20 msimu wa 2020/21 imeendelea kushika kasi huku timu hasimu  za Yanga na Simba zikiendelea kushikana kileleni mwa msimamo wa kundi A.

Timu hizo  kutoka Kariakoo  Dar es Salaam, kila moja imefikisha pointi nne baada ya kushuka uwanjani mara mbili huku Yanga ikiwa kileleni mwa msimamo kutokana na uwaiano mzuri wa mabao.

Baada ya sare katika mchezo wao wa  kwanza Yanga imeibuka na ushindi wa mabao 2-0, dhidi ya JKT Tanzania, mabao yaliyofungwa na Yohana Ndushi  katika dakika ya 68 na Abby Mikimba ambaye alifunga bao la pili katika dakika ya  77 wakati Simba waliibuka na ushindi mwembamba wa bao 1-0 dhidi ya Mwadui katika mechi za juzi.

Akizungumza na gazeti hili kocha mkuu wa Simba, Nico Kiondo, alisema kuwa mwaka huu ni zamu yao kutwaa taji ndio maana kila mchezo wanaoshuka uwanjani wanaupa uzito ili kufuzu hatua inayofuata katika mbio za kulisaka taji ambalo linashikiliwa na Mtibwa Sugar.

Naye kocha mkuu wa timu ya vijana ya Yanga, Said Maulid, alisema kuwa baada ya kulazimishwa suluhu katika mchezo wa kwanza ameyafanyia kazi mapungufu yaliyojitokeza ndio maana amepata ushindi katika mchezo wa pili ambao umewapa nafasi ya kuongoza kundi.

https://www.apps.tsn.go.tz/public/uploads/ac956fe90a23aabcd42484d0596d58cc.jpeg

YANGA leo inashuka katika Uwanja wa Benjamin ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi