loader
Dstv Habarileo  Mobile
Bodi ya Maziwa yapewa mbinu

Bodi ya Maziwa yapewa mbinu

NAIBU Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega ameitaka Bodi ya Maziwa Tanzania (BMT) kuweka mikakati ya upatikanaji wa keni za kubebea maziwa ili kusaidia ukusanyaji wa bidhaa hiyo kwa urahisi nchini.

Alitoa rai hiyo jijini Dar es Salaam jana alipokutana na viongozi na wakuu wa idara kutoka BMT na Bodi ya Nyama Tanzania.

Alisema hivi karibuni katika Bajeti Kuu ya Serikali yapo mapendekezo ya kuondoa Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) kwenye keni za maziwa kwa lengo la kuweka unafuu kwenye bidhaa hiyo.

Alisema lengo ni kurasimisha tasnia ya maziwa na kuongeza fursa za biashara kwa wazalishaji nchini.

Aidha, aliitaka Bodi ya Maziwa kushirikiana na viwanda vya maziwa, Tamisemi na wabia wa maendeleo katika kuhakikisha hamasa kubwa inatolewa ili kuongeza uzalishaji na usambazaji wa keni kwa wingi nchini baada ya kuwapo kwa unafuu unaopendekezwa.

“Bodi ya Maziwa tunataka mshirikiane na viwanda vikubwa, vya kati na vidogo

katika kuhakikisha keni za maziwa zinaenda kwa wingi kwa wadau na hasa akinamama na vijana katika halmashauri zetu nchini,” alisema.

Uliga aliitaka BMT iwashawishi wakurugenzi wa halmashauri na kwa kushirikiana na wataalamu wa Tamisemi wakiwemo maofisa mifugo, maofisa ushirika na maofisa maendeleo ya jamii kuhakikisha asilimia 10 ya mapato ya mifugo inatolewa kwa akinamama na vijana kama mikopo kwa ajili ya tasnia ya maziwa na fedha hizo zisaidie kununua keni na ukusanyaji wa maziwa.

Msajili wa Bodi ya Maziwa Tanzania, Dk George Msalya alisema kwa takwimu zilizopo, takribani asilimia tatu ya maziwa yanayozalishwa nchini yanafika viwandani kwa ajili ya kuchakatwa na hivyo yanayoingia katika mfumo ulio rasmi ni kidogo.

Dk Msalya alisema hali hiyo inatokana na kukosekana kwa mifumo mizuri ya ukusanyaji wa maziwa na gharama kubwa ya ununuzi wa vifaa vya kukusanyia zikiwamo keni.

Alisema kwa nafuu inayotolewa, bodi inajipanga keni zipatikane kwa wingi na kuwafikia akinamama na vijana kama alivyoagiza Naibu Waziri huyo.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/0e3ff51fdf3b0f1ad52b7724b8de82fe.jpg

NAIBU Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya ...

foto
Mwandishi: Vicky Kimaro

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi