loader
Dstv Habarileo  Mobile
Komba: Msifungie watoto walemavu ndani

Komba: Msifungie watoto walemavu ndani

KUELEKEA maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika kesho Juni 16, 2021,  yenye kauli mbiu ya ‘Tutekeleze ajenda 2040 kwa Afrika imfaayo mtoto’, Wazazi na Walezi nchini wameshauriwa kutowafungia ndani watoto wenye ulemavu wa aina yoyote ile na badala yake wahakikishe wanaacha watoke nje na kubwa zaidi wapatiwe haki zao za msingi ikiwamo ya elimu.

Hayo yamesemwa leo jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha kupinga ukatili wa kijinsia (CAGBV), Sophia Komba ambapo alisema  watoto wenye ulemavu wakiwezeshwa wanaweza kufanya mambo makubwa yakiwamo ya kutimiza ndoto zao, hivyo kuwafungia ndani ni kuwanyima haki zao za msingi, na kuitaka jamii yenye tabia  wakaiacha.

Alisema  kitendo cha kumfungia mtoto ndani kwa sababu ya ulemavu alionao si jambo nzuri na wala halimpendezi Mwenyezi Mungu kwani mtoto hakuomba kuwa alivyo.

“Pia kumfungia mtoto ndani unamfanya ashindwe kukua kutokana na kukosa miale ya jua na hasa ya nyakati za asubuhi.” alisema na kuongeza

“Nitoe rai watoto wenye ulemavu waachwe wawe huru na wapewe haki zao za msingi ikiwamo elimu ambayo ndio msingi wa maendeleo yake ambayo yatamfanya atimize ndoto yake.Tuwaendeleze watoto wenye ulemavu kufikia malengo yao,” alisema

Kwa upande Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi Kujenga Jamii Jumuishi Tanzania (BISTO), Paschal Majula  alisema changamoto kubwa inayowakumba watoto  wenye ulemavu ni kutumika kama nyenzo ya kujipatia kipato kwa kuwa ombaomba, kufanyishwa kazi za nyumbani, kutupwa watoto wenye ulemavu wakiwa wachanga na  kufichwa majumbani.

Changamoto nyingine ni  kukosa miundo mbinu rafiki inayowafanya washindwe kwenda shule na kupata huduma zingine kama za choo viwanja vya michezo na kunyima lishe bora na kudumaa.

Aidha alisema serikali inapaswa kuifanyia marekebisho sheria ya ndoa ya mwaka 1971 inayoruhusu mtoto chini ya miaka 18 kuolewa kwa ridhaa ya mzazi kama ilivyoamuliwa na Mahakama ya Rufaa katika kesi ya msingi ya dhidi ya Mwanasheria Mkuu wa Serika na Mwanaharakati  Rebeca Gyumi rufaa namba 204 ya mwaka 2019.

Katika kesi hiyo  Mahakama ya Rufaa iliamuru kifungu cha 13 na 17 cha sheria ya ndoa ya mwaka 1971 kinapingana na katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, kwa kuweka umri tofauti wa kuoa na kuolewa kati ya mtoto wa kike na wa kiume ndani ya mwaka mmoja.

“Mpaka sasa hakuna jitihada zozote zilizofanyika katika kutekeleza maamuzi hayo ya mahakama ya rufaa,” alisema.

https://www.apps.tsn.go.tz/public/uploads/b7b36f6dd4d250b72b5472ce33e0cd55.jpg

ALIYEKUWA Mbunge Mteule wa Jimbo la Konde ...

foto
Mwandishi: Vicky Kimaro

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi