loader
Dstv Habarileo  Mobile
Mpango atoa maagizo sita ulinzi wa watoto

Mpango atoa maagizo sita ulinzi wa watoto

MAKAMU wa Rais, Dk Philip Mpango ametoa maagizo sita likiwamo la Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) kuweka mifumo ya kuhakikisha misaada inayotolewa kwenye vituo vya makao na makuzi ya watoto inawafikia walengwa.

Aidha, ameishauri wizara kupitia upya masharti na utaratibu mzima wa kuasili watoto ili kuhamasiaha Watanzania na watu wengine wenye nia njema kuasili watoto.

Dk Mpango alitoa maagizo hayo wakati wa maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika ambayo yamekwenda sambamba na uzinduzi Makao Makuu ya Taifa ya Watoto yaliyopoa Kikombo mkoani Dodoma jana.

Alisema usimamizi wa ufuatiliaji wa baadhi ya taasisi zinazoendeshwa ama kutoa huduma katika vituo vya kutunza watoto, bado si wa kuridhisha.

“Tunazo taarifa za watu wachache ambao wanatumia vituo hivyo kkama fursa ya kujinufaisha wao binafsi. Pia yapo makazi ya watoto ambayo yameanzishwa bila kufuata utaratibu…hivyo natoa maelekezo sita ambayo Wizara ya Afya na kushirikiana na Tamisemi mkayasimamia,” alisema Makamu wa Rais.

Alisema ni vyema kuweka mfumo wa kuhakiki misaada na kwa kufanya hivyo kitadhibiti matumizi yasiyofaa.

“Uwekwe mfumo kwa kudhibiti misaada inayotolewa na wasamaria wema inawafikia walengwa hii itadhibiti matumizi yaasiyofaa ya vituo hivi hususani kwa wale wanatumia vituo hivi kama fursa ya kujinufaisha wao binafsi na hivyo kuwakatisha tamaa wanaotusaidia pale wanapobaini kuwa misaada wanayotoa haiwafikii walengwa,” alisema.

Pia ameelekeza kuwekwa mfumo thabiti wa ufuatiliaji ili kujua nini kinafanyika katika kila kituo ili kuhakikisha malengo ya msingi ya kuanzishwa vituo hivyo yanafuatwa kikamilifu.

Dk Mpango ameelekeza kusimamiwa na kuhakikisha kuwa huduma katika makao ya watoto zinatolewa kwa kuzingatia viwango, matakwa ya sheria na kanuni husika.

“Pia kuwepo na maandalizi ya watoto kurejea katika jamii, mfano kwa kwa kuwachanganya na wenzao katika maeneo mbalimbali kama vile shule, vyuo vya ufundi stadi na kushiriki matukio yanayowahusu watoto,” alisema Dk Mpango.

Agizo jingine nji kuelekeza kusimamia na kuhakikisha makao hayaandishwi kiholela bila kuwa na leseni na kuhakikisha yanakuwa na walezi wa kutosha na wenye sifa stahiki na utoaji wa huduma unazingatia taratibu za kiafya.

Ameelekeza kusimamia na kuhakikisha watoto wanaolelewa kwa kuzingatia mila, tamaduni na desturi za kitanzania.

Aliishauri wizara kupitia upya masharti na utaratibu mzima wa kuasili watoto ili kuhamasisha Watanzania na watu wengine wenye nia njema kuasili watoto hivyo kupunguza idadi ya watoto kwenye makao.

“Nitumie fursa hii pia kuwasihi Watanzania wenye uwezo waguswe na maisha ya watoto wanaoishi kwenye mazingira hatarishi na wachukue hatua kuasili watoto na kuwatunza kwa upendo.

Sheria ya Kuasili Mtoto Sura ya 335 ya mwaka 2002 inayohusu taratibu za kupata cheti cha kuasili, inawataka watu wenye nia ya kufanya hivyo kuwasilisha nakala ya uamuzi kutoka Mahakama Kuu, cheti cha kuzaliwa cha mtoto anayeasili na kulipia ada halisi kwa ajili ya cheti cha kuasili mtoto ambayo kwa sasa ni Sh 100,000.

Dk Mpango alitoa wito kwa Watanzania wote kushirikiana kuhakikisha haki za mtoto zinalindwa na kuchukua hatua pale ambako watoto wananyimwa haki zao.

“Pia niiagize wizara kuimarisha programu ya msaada wa ushauri wa kisaikolojia kwa watoto, familia na jamii katika ngazi zote ili kupunguza athari na changamoto zinazotokea ndani ya familia na jamii zetu kwa ujumla,” alisema.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk Dorothy Gwajima alisema kituo hicho cha Kikombo kimegharimu Sh bilioni 12.7.

Dk Gwajima alisema makao hayo yenye uwezo wa kuhudumia watoto 250 kwa wakati mmoja, yamejengwa kwa ushirikiano kati ya Serikali ya Tanzania na Mfuko wa Abbott ambayo imetoa fedha hizo huku wizara ikigharamia fidia na Halmashauri ya Jiji la Dodoma ikisamehe Sh milioni 665 kama gharama ya ardhi.

Kwa sasa makao makuu yanahudumia watoto 28 ambao watoto 16 ni wa kike na 12 ni wa kiume wenye umri kati ya miaka miwili hadi 17.

Dk Gwajima alisema ujenzi wa makao makuu haya utawezesha kutatua changamoto zilizokuwa zinajitokeza katika makao makuu yaliyokuwapo Kurasini mkoani Dar es Salaam yaliyokuwa na changamoto ya ufinyu wa eneo hivyo kukwamisha baadhi ya shughuli kufanyika kama michezo, bustani, ufugaji na kazi zingine za kuongeza kipato na lishe na afya.

Mwaka huu kaulimbiu ya Siku ya Mtoto wa Afrika inasema, “Tutekeleze Ajenda 2040: kwa Afrika inayolinda haki za mtoto.”

Naye Mkurugenzi wa Abbot Fund Tanzania, Natalia Lebou alisema kwa zaidi ya miaka 20 taasisi yake imeshirikiana na Serikali ya Tanzania hususani sekta ya afya kwa kutoa mafunzo wa watoa huduma na kuimarisha miundombinu na utoaji huduma katika vituo vya kutolea huduma.

Kuhusu kituo hicho alisema taasisi yake  imeamua kushiriki katika ujenzi wa kituo hicho kwa lengo la kuwahudumia watoto walio katika mazingira magumu.

“Tangu mwanzo tulifikiria watoto kuwa na makazi ya muda wakiwa wanajifunza kujitegemea na kuwarejesha mwenye familia na kuendesha maisha yao. Hapa tuna shamba, karakana na sehemu ya kujifunza vitu mbalimbali,” alieleza.

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maendeleo ya Jamii, Constantine Kanyasu alisema kumekuwa na changamoto kubwa ya watoto wa mitaani na wale wenye utapiamlo na kusisitiza kuwa no changamoto zonazotakiwa kushughulikiwa kwa nguvu zote.

Kwa upande wake, Rais Samia Suluhu Hassan aliandika katika mtandao wake wa kijamii wa twitter akisema, “Tunapoadhimisha Siku ya Mtoto wa Afrika, nawasihi wazazi wenzangu na jamii kwa ujumla kutafakari kwa kiwango gani tunatetea haki za mtoto, tunawalinda dhidi ya unyanyasaji na ukatili na tunatimiza wajibu kwa kuwapa malezi bora na furaha. Natawakia kheri watoto wote wa Afrika.”

https://www.apps.tsn.go.tz/public/uploads/1d958555ded8e9d4f216291f991f26e7.jpg

ALIYEKUWA Mbunge Mteule wa Jimbo la Konde ...

foto
Mwandishi: Anastazia Anyimike, Dodoma

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi