loader
Dstv Habarileo  Mobile
Kumekucha Yanga,  Ruvu Shooting leo

Kumekucha Yanga, Ruvu Shooting leo

YANGA leo saa 1:00 usiku itashuka dimbani kuikabili Ruvu Shooting katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara utakaochezwa kwenye dimba la Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.

Mchezo wa mwisho wa ligi kati ya timu hizo, Yanga ilishinda 2-1 dhidi ya JKT kwenye Uwanja wa Jamhuri, Dodoma katika mchezo uliokuwa mkali.

Katika michezo mitano iliyopita, mabingwa hao wa kihistoria wa Ligi Kuu hawakuwa vizuri sana wala vibaya, kwani walishinda michezo mitatu, sare moja na kupoteza mmoja.

Yanga inashika nafasi ya pili ikiwa na pointi 61 katika michezo 29, nyuma ya vinara Simba yenye pointi 67 katika michezo 27.

Mchezo huo ni muhimu kwa vijana hao wa Jangwani kupata ushindi ili kuendelea kuwa katika mbio za ubingwa, ingawa timu wanayokutana nayo sio rahisi kwao kama wataidharau.

Ruvu Shooting ni moja ya timu zisizotabirika na miaka ya karibuni imekuwa ikionesha upinzani mkali kwa Yanga.

Timu hiyo ya Jeshi iko katika nafasi ya 10 ikiwa na  37. Mwenendo wake kwenye mechi tano zilizopita haukuwa mzuri hali inayowapa presha huenda ikashuka nafasi za chini kama itaendelea kupoteza mechi.

Katika michezo mitano iliyopita, imeshinda mmoja na kupoteza minne.

Kwa matokeo hayo, huenda ikaingia kwa presha ya kutafuta matokeo mazuri na kwa kuzingatia pointi walizo nazo hazitoshi kuwahakikishia usalama wao.

 Michezo mingine itakayochezwa leo ni Dodoma Jiji dhidi KMC kwenye Uwanja wa Jamhuri, Dodoma na Mwadui itawakaribisha Mtibwa Sugar mkoani Shinyanga.

Ushindi ni muhimu kwa kila timu ukiacha Mwadui ambayo tayari imeshashuka daraja.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/85256bc9429affd8820199a6d92f4c92.jpg

YANGA leo inashuka katika Uwanja wa Benjamin ...

foto
Mwandishi: Grace Mkojera

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi