loader
Dstv Habarileo  Mobile
JKT yaichapa Ihefu 2-0

JKT yaichapa Ihefu 2-0

JKT Tanzania imeibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Ihefu katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliochezwa jana kwenye Uwanja wa Jamhuri, Dodoma.

Mabao ya washindi yalifungwa na Jabir Aziz na Edson Katanga katika dakika ya nne na nane, ambayo yalidumu hadi mwisho wa mchezo huo.

Ushindi huo unaifanya JKT Tanzania kupanda juu kidogo kutoka nafasi ya 15  hadi ya 11 katika msimamo wa ligi hiyo, ingawa inaweza isidumu kutegemea na matokeo ya mechi nyingine za leo.

Kichapo hicho kinaifanya Ihefu kuwa katika nafasi ya 13 baada ya kucheza mechi 31, ikiwa na pointi 34 na imekuwa ikipigania kutoshuka daraja kwani haiko katika nafasi salama.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/b6c781948589f7099e907175deedcbe2.jpg

YANGA leo inashuka katika Uwanja wa Benjamin ...

foto
Mwandishi: Grace Mkojera

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi