loader
Dstv Habarileo  Mobile
NMB yaunga mkono mkatati wa Samia kukomboa wanawake

NMB yaunga mkono mkatati wa Samia kukomboa wanawake

BENKI ya NMB kupitia Jukwaa la Mwanamke Jasiri imeanza kutekeleza mkakati wa Rais Samia Suluhu Hassan unaolenga kuwakomboa wanawake kiuchumi kwa kuwapatia elimu ya ujasiriamali pamoja na kuwapa mitaji.

Hatua hiyo imekuja siku chache baada ya Rais Samia kumtaja Ofisa Mtendaji Mkuu wa NMB, Ruth Zaipuna kuwa mmoja wa wanawake watakaoshiriki mchakato wa kujadili na kupatia ufumbuzi wa haki za wanawake kiuchumi.

Katika mkutano na wanawake uliofanyika kwenye ukumbi wa Jakaya Kikwete jijini Dodoma Juni 8, mwaka huu ulioshirikisha takribani wanawake 10,000, Rais Samia alisema eneo hilo ni nguzo muhimu katika kuleta usawa wa kijinsia.

“Nawaomba wadau tushirikiane katika hilo. Najua kati yetu hapa nina vijana wazuri kwenye mabenki wakiongozwa na ndugu yangu wa NMB (Ofisa Mtendaji Mkuu, Ruth Zaipuna). Huyu ni mmoja kati ya wanawake niliowachagua watakaoshiriki jambo hili, sambamba na wengine walio kwenye sekta ya uchumi,” alisema Rais Samia.

Katika kuunga mkono mkakati huo wa Rais Samia, NMB imezindua Jukwaa la Mwanamke Jasiri kwa wanawake wote wa mikoa ya Kanda ya Kusini ambalo linalenga kuwainua kiuchumi.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa jukwaa hilo mkoani hapa, Meneja wa NMB Kanda ya Kusini, Janet Shango alisema linalenga kuwawezeshaa wanawake kutatua changamoto mbalimbali za kiuchumi ambazo zinawakabili katika harakati zao za kufanya maendeleo ya maisha yao na taifa kwa ujumla.

“NMB Mwanamke Jasiri imekuja wakati mwafaka kwa sababu mtakumbuka mwaka huu tumepata Rais mwanamke Mama Samia na ameweka mkakati ili kuwawezesha wanawake wa Tanzania kujikomboa kiuchumi,” alisema.

Shango alisema hatua ya Rais Samia kuwapigania wanawake kuinuka kimaendeleo imeongeza chachu na kuwapa nguvu NMB kuwawezesha kupiga hatua zaidi kwenye maendeleo yao na nchi.

Akielezea namna jukwaa hilo litakavyowasaidia wanawake Kanda ya Kusini, Shango alisema linalenga kutoa elimu ya masuala ya kifedha kwa makundi mbalimbali ya wanawake wakiwemo wajasiriamali wa chini, wa kati na wakubwa, pamoja na ambao bado hali zao zipo chini katika kujishughulisha na biashara kwa ajili ya maendeleo.

Alisema jukwaa hilo pia linahusisha wanawake walioajiriwa na wanaojiari katika sekta mbalimbali, ambao pia watafundishwa namna ya kujiwekea akiba za fedha na  namna bora ya kuendeleza biashara wanazofanya.

Katika hatua nyingine, NMB Kanda ya Kusini imekutana na kuzungumza na wafanyabiashara zaidi ya 200 wa mikoa ya Ruvuma, Mtwara na Lindi kwa lengo la kufahamu changamoto zinazowakabili na namna ya kuzitatutua.

Katika warsha hiyo ya siku moja iliyofanyika mjini hapa, uongozi wa benki hiyo uliwaeleza wafanyabiashara hao kuwa imejipanga kuboresha huduma zake kwa kutafuta mbinu mbadala za kuboresha huduma ikiwamo mikopo kwa wafanyabishara.

Mkuu wa Kitengo cha Majanga na Mikopo wa benki hiyo, Oscar Nyirende alisema mbinu hizo ni pamoja na kuhakikisha wanayafikia makundi yote kwenye jamii ili yanufaike na mikopo inayotolewa na benki hiyo.

“Hatua hii ya kuwakutanisha wafanyabiashara inasaidia kufahamu mambo mengi yanayowakabili na benki tutaweza kujua kitu gani tufanye ili kumaliza changamoto hizo,” alisema Nyirende.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/006a33b704e53780c2c26f960c65cee1.jpg

ALIYEKUWA Mbunge Mteule wa Jimbo la Konde ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu, Mtwara

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi