loader
Dstv Habarileo  Mobile
Prado yatelekezwa na Lumbesa  la dawa za kulevya

Prado yatelekezwa na Lumbesa la dawa za kulevya

MAMLAKA ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) kwa kushirikiana na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imekamata kilo 88.27 za dawa ya kulevya aina ya Heroin na Methamphetamine.

Akizungumza leo (Alhamisi), jijini Dar es Salaam, Kamishna wa Mamlaka hiyo, Gerald Kusaya alisema  dawa hizo zimekamatwa katika eneo la  Kimara- Juni 2, 2021, majira ya saba usiku yakiwa yamepakiwa ndani ya gari aina ya Toyota Prado ambalo lilikuwa limetelekezwa barabarani.

Alisema dawa hizo zimekamatwa baada maofisa wa TRA kulitia shaka gari hilo na kuanza kulifuatilia ambapo baada ya dereva wa gari hilo kubaini kuwa anafuatiliwa aliamua kulitelekeza.

"Baada ya dereva wa gari hilo kubaini anafuatiliwa alitelekeza gari na kukimbia, baada ya upekuzi wa kisheria kufanyika ndani ya gari kulipatikana na mifuko mikubwa mitatu aina ya sandarusi (viroba).

"Ndani yake ikiwa na pakiti 12 za dawa za kulevya aina ya Heroine zenye uzito wa kilo 12.25 pamoja na kontena za plastiki 73 ndani yake kukiwa na dawa aina ya Methaphetamine zenye uzito wa kilo 76.02," alisema Kusaya.

Alisema upelelezi bado unaendelea ikiwemo kugundua mmiliki wa gari hilo na mtandao wake na kuongeza kuwa Mamlaka kwa kushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na usalama “viko macho” kukabiliana na biashara haramu ya dawa za kulevya.

"Ama zao, ama zetu lakini watambue Mamlaka tupo kazini muda wote na lengo letu ni kukomesha kabisa biashara hi haramu.
“Tunaomba wananchi waendelee kutoa taarifa ili kwa pamoja tushirikiane kukomesha dawa hizo," alisema.

https://www.apps.tsn.go.tz/public/uploads/7edaabfbf9f0e248347a24c2d3012f9d.jpg

ALIYEKUWA Mbunge Mteule wa Jimbo la Konde ...

foto
Mwandishi: Vicky Kimaro

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi