loader
Dstv Habarileo  Mobile
Ma-DC vijana kuweni wabunifu mmeaminiwa

Ma-DC vijana kuweni wabunifu mmeaminiwa

RAIS Samia Suluhu ameteua wakuu wa wilaya 139 wakiwamo vijana ambao wengine, huu ndio uteuzi wao wa kwanza.

Wengine wamebadilishwa vituo vya kazi kutoka kimoja kwenda kingine. Kati ya walioteuliwa, wapo wanasiasa, wasanii, wabunge wa zamani na wanahabari. 

Uteuzi huu wa Rais Samia umeakisi nia aliyoionesha hivi karibuni wakati akizungumza na vijana wilayani Nyamagana, Mwanza aliposema, anaamini uwezo wa vijana katika kutenda kazi na kuendeleza taifa.

Mbali na kumpongeza Rais Samia kwa nia hiyo ya kuwaamini na kuwapa vijana nafasi zaidi kutumikia taifa, vijana waliochaguliwa wanapaswa kutumikia nafasi hizo kwa weledi, uadilifu, umakini na ubunifu.

Hapa niseme tu kwamba, kila mmoja hana budi kujitambua kuwa sasa si kijana tena, bali ni kijana kiongozi wa umma ambaye kila wanalofikiri, kulisema au kulitenda,linapaswa kuaksi maslahi ya umma likizingatia weledi, ubinifu, umakini na uadilifu.

Hayo ni mambo yatakayowawezesha kutumikia jamii kwa tija zaidi.

Kwa kuwa wengi wa walioteuliwa ni wasomi, wote wazingatie uadilifu na misingi, taratibu, kanuni, miongozo, maadili na sheria za nchi sambamba na utu katika kazi zao.

Ifahamike kuwa, hakuna mahala ambapo mtu anaenda kusomea kuwa mkuu wa wilaya isipokuwa ni elimu hiyo hiyo aliyo nayo mteuliwa sambamba na mafunzo maalumu baada ya mtu kuchaguliwa au kuteuliwa.

Hili pia linahusisha kupenda na kuheshimu kazi uliyodhaminiwa na kukabidhiwa kwa kuwa umakini utafanikisha maendeleo thabiti ya wilaya husika hasa katika usimamiaji na utekelezaji wa mipango iliyokwishawekwa na kutengewa fedha.

Kwa kuwa mmekuwa wakuu wa wilaya (DC), simamieni suala hilo na kwa kufanya hivyo, ni wazi maendeleo zaidi yatapatikana.

Ninaamini Rais Samia na Watanzania wanawaamini na wanatumaini kuona mkiwa wabunifu kwani hilo ni jambo muhimu katika kuleta maendeleo ya watu katika wilaya zenu huku kila mmoja akitambua kuwa, hakuna maendeleo ya watu kama hakuna maendeleo ya vitu zikiwamo huduma za kijamii

Mkiwa wabunifu na kila mmoja kuepuka ubinafsi na badala yake mkashirikiana na viongozi na watumishi wengine katika halmashauri wilayani kwenu, mnaweza kuanzisha hata miradi itakayochagiza maendeleo katika wilaya na kuzitafuatia ufumbuzi kero mbalimbali za wananchi.

Aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe na kuhamishiwa Temeke, Jokate Mwegelo, ameonesha ubunifu mwingi uliomfanya akubalike ndani ya jamii huku akionesha wazi kuleta maendeleo ya watu na vitu wilayani Kisarawe.

Moja ya mafanikio hayo, ni ‘Mpango wa Kutokomeza Zero’ uliosaidia wanafunzi wengi kufaulu na kuondoa zero wilayani humo. Ubunifu kama huo ndio mategemeo ya Rais Samia kwa ma- DC wateule na wengine waote.

Ndiyo maana ninasema, hakikisheni mnazingatia weledi, umakini na ubunifu katika kuongoza ili kazi iendelee kwa ufanisi.

https://www.apps.tsn.go.tz/public/uploads/cf386dc29c4077a1f5e01de23cd0ecc6.jpg

TAARIFA za matukio ya mimba na ...

foto
Mwandishi: Evance Ng’ingo

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi