loader
Dstv Habarileo  Mobile
‘Hamna sababu ya kuchimba madini kwa kubahatisha’

‘Hamna sababu ya kuchimba madini kwa kubahatisha’

WACHIMBAJI wadogo wa madini wamekuwa wakifanya uchimbaji holela na wa kubahatisha, hali inayowafanya wengi kujikuta wakitumia nguvu nyingi, muda mrefu na kupoteza fedha lakini mwisho wa siku wakiambulia patupu.

Ni kwa msingi huo, mratibu wa mafunzo kutoka Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST), John Kalimenze amewataka wachimbaji wadogo mkoani Shinyanga kuachana na uchimbaji holela na uchenjuaji wa makinikia wa kubahatisha.

Kalimenze anasema kuwa uchimbaji holela una madhara yake kwani unasabbaisha uhalibifu wa mazingira kwa kuacha mashimo hovyo mbaali na kutumia nguvu nyingi na muda mrefu pamoja na raslimali fedha.

Ni kwa mantiki hiyo bosi huyo wa mafunzo amewataka watumie sampuli za kitaalamu kupima udongo wanazofundishwa na si kinyume chake.

“GST imebaini kuwepo kwa changamoto zinazowakabili wachimbaji wadogo kuhusu namna bora ya uchukuaji wa sampuli katika maabara. Hii ndiyo nguzo kuu ya utafutaji na uchimbaji wa madini wenye tija na huku mtu akitumia muda mfupi ujiongezea kipato,” anasema Kalimenze.

Kalimenze katika mada ya mwongozo wa namna bora ya uchukuaji wa sampuli za uchunguzi wa madini kwa wachimbaji wadogo anasema serikali imeweka mikakati ya kuwasaidia kwa kuwapa mafunzo ili kusiwepo na   uchimbaji holela na uchenjuaji wa makinikia wa kubahatisha.

“Wachimbaji wadogo hawajui sampuli ya kubaini madini hivyo kuwafanya watumie muda mwingi na kuchimba kiholela sisi tumeona ni vyema wajue uchunguzi wa sampuli na kupeleka maabara. Hapo hawatatumia muda mwingi kuchimba na mazingira yatabaki salama,” anasema Kalimenze.

Anasema kuwa mchimbaji mdogo anatakiwa awe na uelewa hata kidogo wa eneo lenye miamba au udongo wa madini kwani wamekuwa wakikata leseni hata eneo ambalo halina madini.

Anawashauri wachimbaji wadogo wakitaka kupima sampuli ya udongo kujua kama kuna madini sio kuchukua kilo moja ya udogo bali angalau kilo 20 ili mtu apate uhakika kama eneo la linaweza kuwa na madini au la.

Ofisa Madini mkoa wa Shinyanga, Joseph Kumburu, anasema kuwa Tume ya Madini kwa kushirikiana GST wameanza kutoa mafunzo namna ya usomaji wa sampuli kwani kumekuwepo pia na tatizo la udanganyifu wa marudio ya udongo.

Kumburu anasema kuwa mtu anapochukua udongo udhaniwao kuwa na dhahabu hutoa fedha nyingi na matokeo yake hupata gramu kidogo au kutopata kabisa.

Katibu tawala msaidizi mkoani Shinyanga, Gwalugano Mwakanyamala anasema kuwa GST kwa kushirikiana na tume ya madini imekuwa ikijitahidi kufanya kazi kwa ukaribu na wachimbaji wadogo kwa kuwapatia elimu.

Anasema kuwa GST kwa kushirikiana na Tume ya Madini wamekuwa wakijitahidi kufanya kazi kwa ukaribu na wachimbaji wadogo kwa kuwapatia elimu mbalimbali zinazohusiana na masuala ya madini hivyo ni muhimu wachimbaji wadogo kufanyia kazi mafunzo wanayopata.

“Uwepo wa taarifa za kisayansi zinazokusanywa na  kutolewa na GST kupitia tafiti za awali zimekuwa kichocheo kikubwa cha ukuaji wa sekta ya madini na kuchangia pato la taifa. Kwa kwa  mwaka wa fedha 2019/2020  madini yamechagia asilimia 5.2,” anasema Mwakanyamala.

Anasema kuwa serikali inatambua umuhimu wa wachimbaji wadogo kwani zaidi ya asilimia 80 ya watu wote walioajiriwa na sekta ya madini ni wachimbaji wadogo na ndiyo mkombozi wa mwananchi wa kipato cha chini.

Ofisa programu na mtafiti taasisi ya kuendeleza wachimbaji wadogo nchini (FAdev), Evans Rubara anasema kuwa bado wachimbaji wadogo wanakumbwa na changamoto nyingi ingawa sera inawapa unafuu katika ulipaji wa kodi.

Rubara anasema kuwa serikali imefanya mengi kwa wachimbaji wadogo ila hawajawezeshwa vilivyo kupata maeneo yaliyofanyiwa utafiti wa kijiolojia ili waweze kunufaika zaidi.

Rubara anasema wachimbaji wadogo wamekuwa wakisema kuwa maeneo mengi hayajafanyiwa utafiti na kutambulika kama kuna madini pia hawajui ni kina gani wakichimba kinaweza kuwa na madini, hivyo wamekuwa wakichimba kiholela na kubahatisha.

“Wachimbaji wadogo wamekuwa wakitumia pesa nyingi na ndio changamoto kubwa kwao, wanalipa ushuru ila hawajafanyiwa makadirio kwa uchunguzi uliofanyika  na hivyo kuna upotevu mkubwa wa mitaji yao. Hivyo wanatakiwa kupatiwa elimu juu ya utafiti kubaini madini yalipo,” anasema Rubara.

Emanuel Masanja, meneja mgodi wa Tambarare uliopo Halmashauri ya Msalala wilayani Kahama mkoani Shinyanga anashukuru sana kuhusu mafunzo hayo.

Anakiri kwamba eneo hilo linye wachimbaji zaidi ya 300 wamekuwa wakiendesha uchimbaji wao kwa kubahatisha na ni wa holela.

 

0788 717981

Masanja anasema kuwa uchimbaji wa namna hiyo ndiyo unawafanya wachimbe mashimo yenye kina cha zaidi ya mita 300 kwenda chini lakni wakati mwingine wakiambulia patupu kutokana na kukosa elimu ya kufanya utafiti.

Baadhi ya wachimbaji wadogo, Pius Shilinde na Rehema Mushi wanasema wamekuwa wakishindwa kutambua mwamba na kilichomo kwenye makinikia na ndiyo maana kumekuwepo na uharibifu wa mazingira kwa uchimbaji holela.

Rehema anasema kuwa kukosana kwa elimu ya utambuzi wa sampuli katika maeneo yenye madini wamekuwa wakitumia njia za kienyeji hivyo wanaipongeza GST kwa kuwapa elimu.

 

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/ea2046c688a8e1c72bf640f8d2bbf84a.jpg

OFISI ya Taifa ya Ukaguzi (NAOT) ni Taasisi ...

foto
Mwandishi: Kareny Masasy

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi