loader
Tuunge mkono vita dhidi ya uovu nchini

Tuunge mkono vita dhidi ya uovu nchini

WIMBI la matukio yanayohatarisha maisha ya watu na usalama wa nchi yamezidi kuongezeka siku hadi siku, huku kasi ya mabadiliko ya teknolojia yakichagiza mbinu mpya za uhalifu kama zinavyobuniwa mbinu za kuukabili.

Katika vyombo vya habari yakiwamo magazeti, kwa siku za hivi karibuni kumekuwa na taarifa za kusikitisha za ongezeko la mauaji ya kinyama kwa watoto kunyongwa, binti kuumua kwa kumchoma visu mama yake anayemlea, kijana msaidizi wa kazi za ndani kumua bosi wake na watoto na mengineyo.

Aidha, ukiacha matukio hayo, Juni 21 basi dogo lililokuwa limeweka mashada ya maua kudanganya limebeba msiba kumbe si kweli lilipata ajali likuhisusha magari mengine mawili katika eneo la Nane Nane mkoani Morogoro na kusababisha vifo vya watu tisa.

Kama hiyo haitoshi, usiku wa kuamkia juzi, polisi mkoani Morogoro walikamata mabasi sita yakisafirisha abiria yakiwa na mashada ya maua kuashiria yanasafirisha majeneza yenye miili ya marehemu wakati ni uongo ili tu wasikaguliwe na askari wa usalama barabarani.

Lakini pia, juzi Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu, Jenista Muhagama alikaririwa akisema serikali imebaini mbinu za usafirishaji dawa za kulevya ikiwamo kutumia mananasi.

Jenista alieleza hayo bungeni, Dodoma alipokuwa akitoa taarifa ya hali ya dawa za kulevya kwa mwaka 2020 ikiwa ni matakwa ya sheria inayotaka Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya iandae na kuiwasilisha bungeni taarifa ya hali ya hali ya mapambano hayo kila mwaka.

Hayo niliyoyaeleza ni sehemu tu ya mambo na matukio yanayoendelea nchini yakionesha kuendelea kwa kasi ya maovu katika jamii. Nani asiyefahamu athari za dawa za kulevya kwa vijana ambao ndio nguvu kazi ya taifa.

Ni uongo wa namna gani huu wa kuweka mashada ya maua kwenye gari mbele karibu na dereva ili tu askari wa usalama barabarani wasiwakague wakijua wahusika mmebeba maiti kuelekea kuzika.

Uongo huu unaopimwa kwa mizani ya kifo cha uongo cha mtu ni hatari kubwa sana kama kumpima Mungu wakati vitavu vitakatifu vinakataa kumjaribu Mungu.

Ebu fikiria watu wanaweka dawa za kulevya katika mananasi, matunda yaliozoeleka kuwa mlo wenye kuleta afya, sasa yanatumika kubeba vitu vinavyomuangamiza mwanadamu bila huruma, hofu wala utu.

Matukio haya machache kati ya mengi yanayofanywa ni hatari kwa usalama wa raia na nchi, hivyo hayapaswi kuangaliwa kwa jicho moja na kuiachia Polisi au vyombo vya ulinzi na usalama pekee, bali inahitaji nguvu ya pamoja ya jamii nzima kupambana.

Nguvu hiyo inaanzia katika malezi ngazi ya familia. Ukimlea mtoto katika maadili mema ya kuwa na hofu ya Mungu, hata akija kukengeuka ni rahisi kurejea katika mstari na kukataa uovu.

Mtoto arejeshwe kulelewa na jamii nzima na wazazi wanapotaarifiwa kuhusu tabia mbaya za watoto wao, badala ya kuwalinda na kuyafumbia macho maovu hayo, wawajabishe na jamii ihusike kutoa adhabu hizo. Hii inatoa pia ujasiri wa kukemea uovu popote pale mtu atakapokuwa.

Tukifanya hivi tutapunguza matukio haya na nchi yetu itakuwa salama na kwa wale wataobaki kuwa sikio la kufa, wataangukia kwenye mikono ya sheria.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/89ef4a91953992082a0a42de73ea0fba.jpeg

NIPO nyumbani kwa Baba na Mama Chichi. ...

foto
Mwandishi: Gloria Tesha

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi