loader
Tunaanzisha shule za michezo

Tunaanzisha shule za michezo

SERIKALI imesema ipo kwenye hatua za mwisho za kuanzisha shule maalum za michezo, za msingi na sekondari, katika mikoa yote nchini lengo likiwa ni kuwa na shule na vituo maalum vya kuendelezea vipaji vya michezo (sports academies).

Akizungumza kwenye Sherehe za kufunga mashindano ya Michezo na Taaluma kwa Shule za Sekondari (UMISSETA) mjini Mtwara, Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo, Innocent Bashungwa amese Shule hizi zitakuwa zinalea na kuendeleza vipaji vya michezo mbalimbali, na Serikali itakuwa inasimamia kwa ukaribu, kuhakiksiha kuwa vituo vya michezo vya shule za msingi na sekondari, vinapatiwa mahitaji muhimu yatakayo saidia katika kuendeleza vipaji hivyo.

Amesema Serikali kupitia Chuo cha Maendeleo ya Michezo – Malya, inaanzisha kituo maalum cha michezo cha kuendeleza vipaji (Centre of Sports Excellency), kitakachokuwa kinapatikana kutokana na mashindano haya, na maeneo mengine mbalimbali nchini.

"Chuo cha maendeleo ya michezo Malya kimeanzisha mafunzo ya astashahada, ili kupanua wigo wa wanufaika wake, pia kimefungua kituo cha mafunzo Dar es salaam na Ruvuma, ili kusogeza huduma kwa wananchi wengi zaidi. Ni matumaini yetu kuwa, kupitia Chuo hiki, tutaweza kupunguza pengo la watalaam, na walimu wa Michezo ambalo tunalo hivi sasa," amesisitiza, Bashungwa.

Katika mashindano ya mwaka huu ya UMISSETA mkoa wa Dar es Salaam umeibuka mshindi wa kwanza wa jumla katika michezo yote.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/19113894bdb74fb150c43fdf3f7df681.jpeg

Aliyekuwa Mkurugenzi wa Mradi wa ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi