loader
Dstv Habarileo  Mobile
Badru: Mtibwa itawashangaza wengi

Badru: Mtibwa itawashangaza wengi

KOCHA wa Mtibwa Sugar,  Mohamed Badru amesema timu yake itawashangaza watu wengi msimu ujao kutokana na mabadiliko, ambayo amedhamiria kufanya kwenye kikosi chake.

Mtibwa Sugar ni miongoni mwa timu kongwe kwenye Ligi Kuu Tanzania Bara, lakini katika misimu ya hivi karibuni imekuwa na mwenendo wa kusuasua kiasi cha kunusurika kushuka daraja msimu uliopita.

Akizunguza na gazeti hili, Badru alisema amefanya mazungumzo na uongozi wa timu hiyo na wamemhakikishia kumpa fungu kwa ajili ya kusajili wachezaji ambao watairudisha timu hiyo kwenye ubora iliyokuwa nao zamani.

“Ni kweli hatukuwa na mwenendo mzuri, lakini baada ya kukabidhiwa timu kuna mabadiliko kiasi yameonekana ila msimu unaokuja nimedhamiria kuibadilisha kurudi kwenye ubora wake, nitasajili wachezaji wenye ubora na wengine nitachukua kwenye timu yetu ya vijana U-20,” alisema Badru.

Kocha huyo ambaye alitua Mtibwa Sugar baada ya kutimuliwa Gwambina FC, alisema kwa muda mfupi ambao amefundisha timu za Tanzania Bara, amejua ugumu uliopo, hivyo analazimika kuiandaa vizuri timu yake ya msimu ujao ili kumudu ushindani.

Alisema kufanya vibaya kwa Mtibwa kulitokana na wachezaji kukosa ari, lakini asilimia kubwa ya wachezaji wa timu hiyo wana uwezo mkubwa na kama wakiandaliwa vizuri wanaweza kufanya vizuri na hata kuwania ubingwa.

Mtibwa Sugar inashika nafasi ya 11 kwenye msimamo ikiwa na pointi 38  katika michezo 32 iliyocheza imesaliwa na mechi mbili kumaliza msimu huu.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/81abdeb1de5e046a162a26f89627bcc0.jpeg

BAADA ya Yanga kuondolewa kwenye michuano ya Ligi ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi