loader
Dstv Habarileo  Mobile
Corona yafika mikoa ya Arusha, Dar, Mwanza   

Corona yafika mikoa ya Arusha, Dar, Mwanza  

RAIS Samia Suluhu Hassan ametangaza kuwa mikoa ya Dar es Salaam, Arusha, na Mwanza tayari ina wagonjwa wa Corona walioambukizwa na wimbi la tatu la virusi vya ugonjwa huo.

Akiongea na wananchi katika Kata ya Kibaigwa, Wilaya ya Kongwa mkoani Dodoma, Rais Samia alisisitiza kuwa wimbi hilo la tatu lililoibuka duniani hivi karibuni, tayari lipo nchini. Alitaka wananchi waendelee kuchukua hatua dhidi ya ugonjwa hatari ambao unaikumba dunia.

“Hili wimbi la tatu liko kwenye nchi na hakuna la kuficha, tayari tuna wagonjwa kwenye mikoa ya Dar es Salaam,  Arusha, Mwanza na mikoa mingine,” amesema Rais Samia.

Pia amesisitiza kuzingatia maelekezo yanayotolewa na maofisa wa afya ili wimbi hilo lisisababishe vifo nchini kama linavyoendelea kusababisha vifo nchi za nje.

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi