loader
Dstv Habarileo  Mobile
TCRA ilivyojizatiti na   ukuaji wa uchumi kidijiti

TCRA ilivyojizatiti na  ukuaji wa uchumi kidijiti

MAMLAKA ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imeweka bayana mpango wa kuwawezesha vijana wabunifu katika Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (Tehama) kuibua bunifu nyingi zaidi zitakazonufaisha uchumi wa nchi. 

Akizungumza na waandishi wa Dar es salaam, Mkurugenzi Mkuu wa TCRA, Dk Jabiri Bakari  anasema kuwa mwelekeo wa uchumi unavutia matumizi makubwa ya Tehama na kusisitiza kuwa vijana wenye ubunifu katika sekta ya mawasiliano wanayo nafasi kubwa ya kuchangia maendeleo ya uchumi wa Taifa. 

“Tupo kwenye zama za kidijiti kwa hiyo mawazo na fikra kwa jinsi walivyo hawa vijana ni tofauti na kipindi cha nyuma. Vijana wanafikiri na kuona vitu tofauti, kwa hiyo ni lazima tuweze kupata mambo mengi kutoka kwao,” anasema.

Akizungumzia changamoto ya usalama mtandaoni wakati huu Tanzania na dunia ikiwa katika mabadiliko makubwa kwenye sekta ya Mawasiliano, Dk Bakari anasisitiza kuwa ni wajibu wa kila mwananchi kwa kushirikiana na TCRA pamoja na vyombo vya ulinzi na usalama kuhakikisha wanakuja pamoja ili kukomesha vitendo vya uhalifu mtandaoni.

Ili Tanzania iweze kufikia azma ya kuwa na uchumi wa kidijiti, usalama wa watumiaji huduma za mawasiliano kwenye mtandao ni suala ambalo Mamlaka ya Mawasiliano inalitilia mkazo.

Anasisitiza kuwa Mamlaka kwa kushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na usalama ipo macho wakati wote kuhakikisha inadhibiti uhalifu mtandaoni kwa kuhakikisha wananchi wanapatiwa elimu stahiki juu ya matumizi salama ya huduma za mawasiliano mtandaoni.

“Mafanikio ni mazuri kwa maana kwamba watu walikuwa wakipata meseji za kitapeli, nataka nichukue muda huu kuwaeleza kwamba serikali iko kazini. Mamlaka na sekta ziko kazini, tunavyozungumza hivi baadhi ya hao matapeli wengi tu wapo kwenye vyombo vya sheria,” anasema.

Mkurugenzi Mkuu anasisitiza kwamba ni muhimu pia wananchi wakashirikiana TCRA pamoja na serikali kwa ujumla kwa kutoa taarifa za wahalifu wa mtandaoni kwa kutuma ujumbe na namba za washukiwa wa utapeli kwenda namba 15040.

Kuhusu zoezi la kuhakiki namba za simu zilizosajiliwa na mtumiaji wa huduma za mawasiliano ya simu, Bakari anasisitiza kuwa ni muhimu kila mtumiaji wa huduma za mawasiliano akahakikisha anahakiki  namba zake zilizosajiliwa kwa kutumia namba za kitambulisho cha Taifa kwa kubofya *106# kisha kufuata maelekezo.

Anasema ni vyema mtu akafuta usajili endapo mtumiaji atabaini kutozitambua. Anasema ili kufuta namba za simu ambazo mtumiaji hazitambui atapaswa kufika kwa wakala wa mtoa huduma za mawasiliano ambae ndie aliyepewa haki ya kufuta namba asizozitambua.

Akizungumzia sababu za mtumiaji wa huduma za mawasiliano kutopewa haki ya kuzifuta namba za simu alizobaini kutozitambua kwenye simu yake, Mkuu wa Kitengo cha Watumiaji wa Huduma za Mawasiliano cha TCRA, Thadayo Ringo anasema kuwa hatua hiyo inalenga kumlinda mtumiaji.

Anafafanua kwamba zoezi la kufuta namba hizo linahitaji kuchukua alama za kidole ili kuthibitisha kwamba anayetaka kufuta namba ambazo hakuzitambua au ambazo asingependa kuendelea kuzimiliki.

Mkurugenzi Mkuu anabainisha pia kwamba TCRA inaweka mazingira wezeshi kuhakikisha sekta ya mawasiliano inakuwa na mchango mkubwa katika ukuaji wa uchumi wa nchi.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/19fbfa0434e28a7aa2f5b9947ead7ea4.png

OFISI ya Taifa ya Ukaguzi (NAOT) ni Taasisi ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi