loader
Dstv Habarileo  Mobile
Messi akubali kubaki  Barcelona

Messi akubali kubaki  Barcelona

LIONEL Messi amekubali kubaki Barcelona kwa mkataba utakaomuweka mpaka mwaka 2026 utakaohusisha pia kupungua kwa mshahara wake nusu ya aliokuwa akipata mwanzo.

Hilo linategemea na kama mchezaji huyo ataamua kuondoka hivyo Barca itakuwa na uwezo wa kukata mshahara wake.

Messi, 34,alikuwa huru baada ya kumaliza mkataba wake, taarifa zinasema alikuwa akilipwa pauni milioni 123. Mkataba ulimaliziak Juni 30 mwaka huu.

Kwa sasa yuko mapumzikoni baada ya kushinda kombe la Copa America hivyo taratibu za mwisho za kimkataba bado hazijakamilika.

Mkataba huo una kipengele cha kuuvunja kumruhsu Messi kuondoka klabuni hapo baada ya miaka miwili kama atataka.

Kumsajini Messi ilikuwa ni malengo na ahadi za mwenyekiti mpya Joan Laporta.

Barca pia inawania kuwasajili msambuliaji Antoine Griezmann na kiungo wa Atletico Madrid Saul Niguez wote ikiwa na kipengele cha kupunguza mshahara.

Baada ya kushinda Copa America, Messi alijihisi kuwa na nguvu zaidi na kuanza kufikiria kubaki klabuni kwa muda mrefu.

Baada ya miaka miwili anaweza kuvunja mkataba, lakini kama bado atahitaji kuendelea basi ligi ya Marekani MLS itabidi isubiri.

Messi amekuwa akihusishwa na kutaka kuhamia Paris St-Germain na Manchester City ambapo angeungana na bosi wake wa zamani Barcelona Pep Guardiola.

Messi ndio mfungaji bora wa Barcelona mpaka sasa akiweka rekodi ya kufunga mabao 672, ameshinda mataji 10 ya La Liga, manne ya Ligi ya Mabingwa, saba ya Copa del Reys huku akitwaa tuzo ya Ballon d'Or mara sita.

https://www.apps.tsn.go.tz/public/uploads/fbf6582f0ff95bc391f9ee98e31d58ee.jpg

Mambo yamaenza kuvurugika kunako klabu ya PSG, baada ...

foto
Mwandishi: BARCELONA, Hispania

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi