loader
Dstv Habarileo  Mobile
Mafuta ya kupikia yatumika kuzuia uporaji Afrika Kusini 

Mafuta ya kupikia yatumika kuzuia uporaji Afrika Kusini 

WAFANYAKAZI wa maduka makubwa nchini Afrika Kusini katika miji ambayo ina ghasia za uporaji, wameamua kutumia mbinu ya kumwaga mafuta ya kupikia katika milango ya kuingia katika maduka yao ili waporaji wateleze na kushindwa kuingia kwenye maduka yao.

Mbinu hiyo inatumiwa katika maduka ya mji wa Tugela uliopo KwaZulu-Natal, jimbo ambalo kwa siku kadhaa kumekuwa na uporaji katika maduka, maghala na viwanda.

Meneja wa duka moja katika mji huo, Mduduzo Sikhakhane alisema hiyo ni mbinu ya kuzuia waporaji wasiingie dukani.

"Hakuna aliyeweza kuingia dukani kwa sababu walikuwa wanateleza kama wendawazimu," alisema.

Iliripotiwa kuwa hilo ndio duka pekee ambalo halikuvamiwa katika eneo hilo.

Uongozi wa Shoprite ulisema unarekebisha maduka mengine yaliyoathirika na uporaji na kuanza kuweka bidhaa tena.

Ghasia hizo zilianzia Jimbo la KwaZulu-Natal na Gauteng baada ya Rais wa zamani wa Afrika Kusini kufungwa gerezani kwa miezi 15 kwa kosa la kudharau Mahakama.

Watu 72 wamefariki na zaidi ya  1,700 wamekamatwa katika maandamano makubwa kutokea katika miaka kadhaa iliyopita.

Kwa mujibu wa kiongozi wa KwaZulu-Natal, Sihle Zikalale, jimbo hilo linakadiriwa kupata  hasara ya dola za Marekani milioni 206.

https://www.apps.tsn.go.tz/public/uploads/d9d79f34365ff4edf563da1860d2cce9.jpg

Waziri wa Uingereza, Boris Johnson ametengua uteuzi wa ...

foto
Mwandishi: KWAZULU-NATAL, Afrika Kusini

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi