loader
Dstv Habarileo  Mobile
Ziara ya Samia Burundi iimarishe uhusiano wetu

Ziara ya Samia Burundi iimarishe uhusiano wetu

RAIS Samia Suluhu Hassan jana alimaliza ziara rasmi ya siku mbili ya kiserikali nchini Burundi. Rais Samia alikuwa nchini humo kwa mwaliko wa Rais wa nchi hiyo, Evariste Ndayishimiye.

Akiwa nchini humo, alifanya mazungumza na mwenyeji wake, Rais Ndayishimiye, ambapo katika mazungumzo yao walikubaliani takribani katika mambo tisa yenye lengo la kuimarisha uhusiano wa kidugu, biashara, uwekezaji, usalama na mambo mengine.

Aidha, kabla ya kujejea nchini jana, Rais Samia alihutubia Jukwaa la Wafanyabiashara wa Tanzania Burundi katika mji mkuu wa nchi hiyo, Bujumbura kuhusu masuala mbalimbali yanayohusu fursa za biashara na uwekezaji baina ya Tanzania na Burundi. Kwetu sisi, ziara hiyo ya Rais Samia nchini Burundi na nyingine alizozofanya awali katika nchi nyingine jirani za Kenya na Uganda, ni hatua nzuri kwa kiongozi huyo kuimarisha uhusiano wa kidiplomasia, kiuchumi, biashara, kiutamaduni na kijamii na mataifa jirani ambayo ni ndugu na wabia wa maendeleo wa muda mrefu.

Ni matarajio yetu kuwa, ziara ya Rais Samia nchini Burundi itafungua fursa mpya za biashara na uwekezaji baina ya mataifa hayo mawili jirani na rafiki wa muda mrefu.

Ikumbukwe, Burundi ni miongoni mwa washirika wakubwa wa kibiashara wa Tanzania, ambapo kwa mujibu wa takwimu, kampuni 17 za Tanzania zimewekeza Burundi katika sekta ya ujenzi, fedha, afya, usafirishaji na madini, huku 18 za Burundi zikiwa zimewekeza nchini katika sekta mbalimbali.

Takwimu hizo zinaonyesha jinsi nchi hizo zinavyofanya biashara kwa usawa, ingawa jitihada zaidi zinahitajika kuwekeza katika maeneo mengi ambayo hayajafanyiwa kazi. Kwa kutambua umuhimu wa biashara miongoni mwa mataifa hayo mawili, wakati akizungumza na Jukwaa la Wafanyabiashara wa Tanzania na Burundi jana, Rais Samia aliagiza kuondolewa kwa vikwazo vyote vinavyokwaza biashara kati ya Tanzania na taifa hilo.

Hivyo, ziara hiyo ya Rais Samia ni muhimu kwa mataifa hayo mawili ni muhimu sit u katika kuimarisha mahusiano ya kidiplomasia, bali pia kutengeneza mazingira mazuri na rafiki ya kibiashara ili kukuza uchumi wa mataifa hayo kwa faida ya wananchi.

Ziara ya Rais Samia nchini Burundi kwa mara nyingine imedhihirisha nia yake ya kuvutia wawekezaji kuwekeza Tanzania na jitihada zake za kuhakikisha kunakuwa na mazingira bora kwa wawekezaji wan je kuja kuwekeza nchini wa wa nchini kwenda kuwekeza nje. Bila shaka ziaara hiyo imeaimarisha uhusiano mwema uliopo kati ya Tanzania na Burundi na mataifa mengine jirani.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/64c9698e22bebf0d93054f90648d3afd.jpeg

Miradi ya Maendeleo katika halmashauri za Serengeti, ...

foto
Mwandishi: Mhariri

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi