loader
Dstv Habarileo  Mobile
Makali ya tozo na umuhimu wa maendeleo yetu wananchi

Makali ya tozo na umuhimu wa maendeleo yetu wananchi

TOZO mpya kwenye miamala ya simu imekuwa gumzo nchini mwetu tangu ilipoanza kutumika Alhamisi ya Julai 15 mwaka huu.

Ni kweli, tozo hii ina makali yake, ambayo hata mimi ninapojitosa kuijadili inaning’ata lakini bado ninaamini ni kodi sahihi, yenye lengo zuri. Hofu yangu kila nikipitia mijadala mingi kwenye mitandao kuhusu tozo hii, haioneshi upande wa pili wa manufaa yake, hali inayonifanya niamini kwamba watazania wengi hawaelewi kwa nini serikali ikaja na tozo hii.

Kutokana na malalamiko ya wananchi, kuna masuala mengi ya kujiuliza ambayo ukifuatilia hoja za watu unakosa jibu la moja kwa moja na kuibua maswali kama haya; Je, kinachopingwa na ukubwa wa tozo hii kwa mtu anayefanya muamala hasa wenye pesa nyingi, au wanataka itolewe kabisa.

Je, wanaipinga kwa vile hawajui inakwenda kufanya nini au kwa vile hawana uhakika kama itatumika ipasavyo kwa maana ya kwamba wanahisi inakwenda kuwanufaisha wachache?

Kama inavyodaiwa kwamba Watanzania tuna shida katika mikopo na kuihudumia, tunadaiwa pia kwamba hatuna uzalendo wa kupenda na kuona fahari kulipa kodi. Je, hatua hii ya kupinga tozo hii inatokana na kasumba yetu hiyo? Kuna wanasiasa wengi, hususani wa upinzani wameonekana wengi kuipinga tozo. Je, wanachokisema ni mtazamo wao chanya kwa maendeleo ya nchi hii au wanafanya hivyo kwa malengo ya kisiasa?

Kwamba kazi yao ni kupandia kokote ambako watapata kuungwa na mkono na wananchi hata kama na wao leo wakipewa nchi hawatakuwa na namna ya kupata pesa za kuwaletea wananchi mandeleo isipokuwa kupitia kodi na tozo kama hizi.

Kuna wengine wanaona kama tuna raslimali nyingi kama misitu, madini, mbuga za wanyama na kadhalika na hivyo wanahoji kwa nini tumeshindwa kuzitumia hizi kutufikisha tunakotaka bila kuja na tozo kama hizi?

Juzi nilimsikia Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Mwigulu Nchemba akisema Rais Samia Suluhu Hassan ameagiza Wizara ya Fedha ifanyie kazi malalamiko ya wananchi kuhusu tozo hiyo. Ilielezwa kwamba, jana wakati ninaandika makala haya, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alikuwa anatarajiwa kufanya kikao ili kujadili suala hilo.

Mantiki ilinitaka, kabla ya kuandika makala haya, nisubiri kikao hicho lakini nikakumbuka kwamba mimi kama Mtanzania nina haki pia ya kikatiba kutoa maoni yangu kuhusu suala hili ni kama yatawapendeza wakubwa wanaweza kuyatumia ama kuyaacha.

Msimamo wangu, baada ya kuangalia malengo ya tozo hii ambayo ni muhimu sana kwa maendeleo yetu, ninaiunga mkono mia kwa mia, lakini ukubwa wake, hususani kwa miamala mikubwa ndio ingepunguzwa. Nitatoa mapendekezo yake baadaye. Rais wa Awamu ya Nne, Jakaya Kikwete, alisema kwamba huwezi tu kutaka kula bila kuliwa kidogo, hivyo na sisi waanchi tunapaswa kujua kwamba maendeleo yoyote yana gaharama zake hayaji hivi hivi.

Kuna msemo pia kwamba hakuna matamu bina kuvuja jasho na pia kuna hii methali kwamba: ‘Ukione vimeelea, vimeundwa.’ Miradi inayotarajiwa kutekelezwa kutokana na fedha hizo imeelezwa kwamba ni pamoja na ujenzi wa barabara za mijini na vijijini, upatikanaji wa maji safi na salama, afya na bima ya afya kwa wote, elimu na miradi ya kimkakati kama Ujenzi wa Bwawa la Kufua Umeme wa Maji la Mwalimu Nyerere na ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR).

Dk Nchimbi aliweka wazi kwamba ukiondoa kodi kama hizo za miamala ambazo watu wanalipa bila kuandikishwa (indirect tax), idadi ya walipa kodi walioandikishwa ni wachache mno nchini. Alisema walipa kodi wakubwa ni 504 tu kati ya watu milioni 60.

Kwa hiyo akasema ili kuondokana na utegemezi wa nje na kuanzisha miradi inakayofika mwisho na kuwa chachu ya maeneleo katika nchi yetu lazima vipatikane vyanzo zaidi vya mapato ya saerikali, Kwa mapendekezo yangu, pamoja na kutoa elimu kuhusu umuhimu wa kodi hii, wahusika wangeangalia, kwa mfano, Watanzania wengi kwa wastani wanafanya wa miamala ya kiasi gani hasa, labda tuseme kuanzia Sh 1,000 hadi milioni tatu.

Kama ndivyo, basi kiwango cha miamala itakayoonekana ndio inafanywa na wengi, kingepunguzwa. Kisingezidi Sh 2,500. Baada ya mapendekezo yangu, sasa nijaribu kujibu baadhi ya hoja ninazosiona kwenye mitandao kwa mujibu wa uelewa wangu.

Kwa wale wanaodhani kwamba tuna raslimali nyingi kama madini na uwekezaji mbalimbali unaofanyika nchini, ninapenda niwafahamishe wajue pia kwamba miradi mingi ya uwekezaji nchini, inameletwa na mitaji na utaalamu kutoka nje. Kwa hiyo hata kama tunapata bado si kukubwa sana kwa sababu hatuna utalaamu.

Je, tutafikaje kwenye utalaamu na kuwa na miradi mikubwa itakayotusaudia kuijitegemea? Ni kupitia tozo kama hizi ambazo zitahukakishia miradi muhimu kama ya umeme wa maji, reli ya kisas, barabara za mijiji na vijijini, maboresho katika afya na kadhalika.

Ilielezwa kwamba serikali inahitaji takribani shilingi trilioni nne kutoka kwenye tozo hizo za miamala ya simu na zile zilizoongezwa kwenye petrol, dizeli na mafuta ya taa ili kusaidia utekelezaji wa bajeti yake. Kwa hiyo hizi pesa zinahitajika na hivyo ninawashauri wanasiasa wa upinzani, kutumia wachumi wao basi kuisaidia serikali ni wapi itapata fedha hizo kama itaachana na miamala.

Rais Samia alipata kusema jambo jema sana kwamba serikali yake haikatai kukoselewa lakini anayekosoa basi atoe na suluhisho linalotekelezeka.

Ni vyema katika hili, wakati viongozi wetu wakikuna kichw akuhusu cha kufanya, ni vyema kama alivyosema msemaji mmoja: tuache harakati kwenye maendeleo ya watu. Hayupo Mjomba wala shangazi wa kutujengea barabara, shule, zahanati na hospitali kwa ajili yetu. Ni sisi wenyewe.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/7c9ff0b31126716eacd369f399f10c33.PNG

OFISI ya Taifa ya Ukaguzi (NAOT) ni Taasisi ...

foto
Mwandishi: Hamisi Kibari

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi