loader
Dstv Habarileo  Mobile
SMZ yapania mageuzi zao la karafuu

SMZ yapania mageuzi zao la karafuu

SERIKALI ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) inakusudia kufanya mageuzi makubwa ya kilimo cha karafuu kwa lengo la kuona walengwa wananufaika na kupiga hatua ya maendeleo ya kiuchumi.

Hayo yalisemwa na Makamu wa Kwanza wa Rais, Othman Masoud Othman wakati alipozungumza na wananchi na viongozi wa chama hicho Micheweni Pemba katika ziara zake za kikazi.

Alisema wakati umefika sasa kuona wakulima wananufaika na uzalishaji wa kilimo cha karafuu kwa kuleta mabadiliko makubwa ya kiuchumi ambayo yatasaidia kuimarisha maisha yao.

Aliyataja baadhi ya mabadiliko hayo ni kuona ujenzi wa viwanda zaidi vya kusarifu vitakavyoongeza thamani ya zao la karafuu na wakulima kupata fedha nyingi zaidi kutokana na uzalishaji wa bidhaa nyingine.

Aidha, aliitaja mikakati mingine ni pamoja na kuimarisha mashamba ya karafuu ikiwemo kuotesha mikarafuu mipya kuchukua nafasi ya ile iliyozeeka ambayo uzazi wake umeanza kupungua.

“Hayo ni baadhi ya mageuzi makubwa ya kilimo cha karafuu tunayoyakusudia kuyafanya katika kipindi kijacho katika Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar,” alisema.

Mapema Othman aliwataka wakulima wa zao la karafuu kuendelea kuuza karafuu zao katika Shirika la Taifa la Biashara (ZSTC) ambapo safari hii wameweka utaratibu mzuri wa kuhakikisha wakulima wanapata malipo katika mfumo mzuri unaofahamika ambao ni salama.

Aidha, aliwataka wakulima kuachana na magendo ya karafuu ambayo kwa kiasi kikubwa huwaingiza wakulima katika hasara kubwa wakati karafuu hizo zinapokamatwa ambapo hutaifishwa kwa mujibu wa sheria.

“Wito wangu kwa wakulima wa karafuu kuhakikisha wanauza mazao yao kupitia Shirika la Taifa la Biashara (ZSTC) na kuachana na biashara ya magendo ambayo athari zake ni kubwa,” alisema.

Baadhi ya wakulima wa karafuu wamepongeza uamuzi uliochukuliwa na serikali wa kulipa malipo ya fedha kupitia njia ya miamala ya huduma za simu au katika benki ambapo huepusha matukio ya wizi na uporaji.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/2ff06a9dfca7905f3313b520f450fc9c.jpg

SHIRIKISHO la Wafanyabiashara na wenye viwanda nchini ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu, Zanzibar

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi